Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Tulia achaguliwa naibu spika ‘nitawalinda wabunge vijana’
Habari za Siasa

Dk. Tulia achaguliwa naibu spika ‘nitawalinda wabunge vijana’

Dk. Tulia Ackson, akiapa baada ya kuthibitisha na Bunge kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Spread the love

NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson amesema, atawapa kipaumbele na kuwalinda wabunge vijana waliokuwepo na waliongia kwa mara ya kwanza bungeni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Tulia amesema hayo leo Alhamisi tarehe 12 Novemba 2020 wakati akiomba ridhaa kwa wabunge wa Bunge la 12 jijini Dodoma ili wampigie kura kwenye nafasi ya naibu spika licha ya kuwa mgombea pekee kwenye nafasi hiyo.

Mara baada ya kumaliza kujinadi akiwaomba wamchague kwenye nafasi hiyo aliyokuwa akiishikilia katika Bunge la 11 lililomaliza muda wake, Mbunge wa Kasulu Vijijini (CCM), Augustine  Holle alimuuliza swali.

Holle ametaka kujua kuhusu uwepo wa wabunge wengi vijana kwa sasa nawa zamani jinsi ataweza kuwalinda ili waweze kuwakilisha michango ya wananchi waliowachagua.

Wakati wa kujibu swali hilo, Dk. Tulia amesema, yeye akiwa kama msaidizi wa Spika atahakikisha anawahudumia wote wa zamani na wapya ili waondoe wasiwasi katika kuwakilisha michango yao mbalimbali.

Dk. Tulia Ackson

“Bunge lina makundi na rika mbalimbali na niwajibu wangu kama msaidizi wa Spika kuwahudumia kwa kuwawakilisha mawazo ya wananchi waliowachagua na kuwatuma na mimi nitahakikisha nitawalea hawa vijana na wasiwe na wasiwasi,” amesema Dk. Tulia ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini (CCM).

Akijibu swali la Mbunge wa Nkasi Kaskazini (Chadema), Aida Khenani aliyetaka kujua suala la muda kwa wabunge kuchangia bungeni akatavyokabiliana nalo amesema, wabunge wananafasi ya kubadilisha kanuni mbalimbali hasa kanuni ya muda ili waweze kupata fursa zaidi ya kupata muda wa kuchangia mambo mablimbali, kama wataona.

Baada ya kumaliza kujinadi, upigaji kura ulifanyika ambapo, Spika Job Ndugai ametangaza matokeo akisema, wapiga kura walikuwa 354 hakuna kura iliyoharibika. Safari hii ni Bunge la wasomi tupu. Kura za hapana ni nne, kura za ndiyo ni 350.”

Bunge la Tanzania

Mara baada ya kuchaguliwa Tulia aliwashukuru wabunge hao kwa heshima waliyompa na ameahidi kufanya kazi kwa uaminifu kwa kuishauri na kuisimamia Serikali kama ilivyo wajibu wa Bunge.

“Nichukue fursa hii kuwashukuru kwa heshima hii mlionionyesha siku hii ya leo, lakini ni washukuru wananchi wenzangu wa Mbeya Mjini kwa kunipa fursa hii na nahaidi kufanya kazi kwa uaminifu kwa kumshauri spika,” amesema

“Ila sisi kama Bunge tunawajibu wa kuishauri na kuisimammia serikali katika mambo mbalimbali nashukuru tena kwa kura mlizonipa ni wazi kuwa sisi wote ni wabunge na tungeweza kuwa katika nafasi hii ila mliamua kunipa heshima,” amesema Dk. Tulia

Mara baada ya kuchagulia na kutoa shukrani hiyo Spika Ndugai alimuapisha Dk Tulia kisha kuahirisha shughuli za Bunge hadi kesho Ijumaa tarehe 13 Novemba 2020 saa 3:00 asubuhi ambapo Rais John Pombe Magufuli atakapolizindua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!