Dk. Hussein Mwinyi, mgombe wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM akichukua fomu ya kuwania nafasi hiyo

Dk. Mwinyi: Tuache mazoea, tutafute kura

Spread the love

DAKTARI Hussein Mwinyi, mgombea wa urais visiwani Zanzibar, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amewataka viongozi wa chama hicho visiwani humo ‘kuacha mazoea.’ Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Amesema, mazoea ya kwamba watashinda tu, hayapaswi kuendelea na badala yake, amewataka kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wanashawishi wananchi kupiga kura ili ashinde kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

Dk. Mwinyi ametoa kauli hiyo leo Jumatano tarehe 26 Agosti 2020, baada ya kuchukua fomu ya kuomba uteuzi katika Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) visiwani humo.

Dk. Mwinyi anatarajiwa kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Maalim Seif Sharif Hamad, mgombea urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo visiwani humo.

Kwenye uteuzi wa Dk. Mwinyi, kambi ya Maalim Seif ilieleza kufurahishwa na uteuzi huo kwa madai, ni afueni kwao kuelekea ushindi.

Dk. Mwinyi amesema, “itafika wakati wa kaunza kufanya kazi ya kushinda uchaguzi kuanzia katika ngazi ya shina hadi ngazi ya juu. Ni muda wa kuingia kazini na kujipanga na uchaguzi, nataka niseme kwamba ngazi ya watendaji wa majimbo, wilaya, mikoa mpaka afisi kuu, sasa kazi iwe moja nayo ni kujipanga kushinda uchaguzi unaokuja.”

Dk. Mwinyi amewataka wafuasi na viongozi wa CCM visiwani humo kufanya kazi usiku na mchana hadi siku atakapotangazwa mshindi wa uchaguzi huo.

“Naomba niseme kwamba, sasa tufanye kazi usiku na mchana hadi siku natangazwa kuwa washindi wa uchaguzi nanyi wanachama wa CCM, wapenzi wa chama na wakereketwa tunayo jukumu la kuhakikisha sote tunapiga kura siku ya uchaguzi, asibaki hata mtu mmoja,” amesema Dk. Mwinyi.

“Tusibweteke CCM tuna tabia ya kuona kwamba tushashinda wakati tuna jukumu la kutafuta ushindi, niwaombe safari hii iwe tofauti na wanachama wa CCM sote tukapige kura, mabalozi watendaji wa ngazi zote ingine kazini kuhamasisha watu kupiga kura. Sote tukiingia tutashinda kwa kishindo ili tuijenge Zanzibar,” amesema Dk. Mwinyi.

Mgombea huyo wa CCM amewasihi Wazanzibari kuhubiri amani katika mchakato wa uchaguzi huo, kwa kuwa hakuna maendeleo yanayokuja pasina amani.

“Kwanza ndugu zangu, nataka sisi sote tuhakikishe tunahubiri amani, kila mmoja wetu ahakikishe anahubiri amani bila amani hakuna maendeleo, bila amani hata ibada hatutazifanya hivyo tuhakikishe tunailinda amani tuliyonayo,” amehimiza Dk. Mwinyi.

Dk. Mwinyi amesema, endapo atafanikiwa kuchaguliwa na Wazanzibari kuwa rais wao, ataondoa matabaka ya kila aina, ili kila mtu anufaike na uzanzibari wake.

“…nataka niwahakikishie, nikiwa kiongozi wenu nitahakikisha naondoa matabaka kila aina, matabaka ya upemba na uunguja, ya U-Kusini na U-Kaskazini, nitaondoa matabaka ya dini zetu katika kila eneo ili sote tuwe Wazanzibari na kila mmoja wetu anufaike kwa uzanzibar wake,” ameahidi Dk. Mwinyi.

DAKTARI Hussein Mwinyi, mgombea wa urais visiwani Zanzibar, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amewataka viongozi wa chama hicho visiwani humo ‘kuacha mazoea.’ Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea). Amesema, mazoea ya kwamba watashinda tu, hayapaswi kuendelea na badala yake, amewataka kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wanashawishi wananchi kupiga kura ili ashinde kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020. Dk. Mwinyi ametoa kauli hiyo leo Jumatano tarehe 26 Agosti 2020, baada ya kuchukua fomu ya kuomba uteuzi katika Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) visiwani humo. Dk. Mwinyi anatarajiwa kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Maalim Seif Sharif Hamad, mgombea urais…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!