July 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mwinyi arejesha fomu, asifu demokrasia CCM

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi akirejesha fomu za kuwania Urais wa Zanzibar ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Spread the love

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi amerejesha fomu za kuwania Urais wa Zanzibar ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Dk. Mwinyi ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi alikuwa wa tano kati ya wagombea 26 kuchukua fomu hizo katika Ofisi Kuu za CCM, zilizopo Ugunja visiwani humo tarehe 17 Juni 2020.

Baada ya kukabidhiwa fomu hizo, Dk. Mwinyi alisema asingeweza kuongea lolote na anachofanya, anakwenda kuzipitia fomu hizo na kuona kuna nini anapaswa kukifanya. Kubwa ni kutafuta wadhamini wasiopungua 250.

Leo Jumatano mchana tarehe 24 Juni 2020, Dk. Mwinyi amerejesha fomu hizo huku akizungumza kwa ufupi kuwa, “chama chetu kina demokrasia ya hali ya juu, kila aliyetaka anaruhusiwa.”

Dk. Mwinyi ambaye pia ni Mbunge wa  Kwahani amesema kwa sasa anaacha  mchakato wa ndani wa chama kuendelea.

Wagombea waliochukua fomu ni;

 1. Mbwana Bakari Juma
 2. Ali Abeid Karume
 3. Mbwana Yahya Mwinyi :
 4. Omar Sheha Mussa
 5. Hussein Ali Mwinyi
 6. Shamsi Vuai Nahodha
 7. Mohammed Jaffar Jumanne
 8. Mohammed Hijja Mohammed
 9. Issa Suleiman Nassor
 10. Makame Mnyaa Mabarawa
 11. Mwatum Mussa Sultan
 12. Haji Rashid Pandu
 13. Abdulhalim Mohammed Ali
 14. Jecha Salum Jecha
 15. Dk Khalid Salum Mohammed
 16. Rashid Ali Juma
 17. Khamis Mussa Omar
 18. Mmanga Mjengo Mjawiri
 19. Hamad Yussuf Masauni
 20. Mohammed Aboud Mohammed
 21. Bakari  Rashid Bakari
 22. Hussein Ibrahim Makungu
 23. Ayoub Mohammed Mahmoud
 24. Hashim Salum Hashim
 25. Hasna Atai Masound
 26. Fatma Kombo Masound
error: Content is protected !!