Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mpango: Pato la mtu mmoja mmoja limeongezeka
Habari za Siasa

Dk. Mpango: Pato la mtu mmoja mmoja limeongezeka

Spread the love

SERIKALI imeeleza kuwa, pato la wastani la kila mtu kwa mwaka 2018 lilifikia Sh. 2.4 Milioni (2,458,496), kutoka Sh. 2.3 (2, 327,395) mwaka 2017. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Hii maana yake ni kuwa, pato la mtu mmoja mmoja kwa siku limeongezeka kutoka 6,376.4 mwaka 2017 hadi 6,735.6 kwa mwaka 2018.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 13 Juni 2019 bungeni jijini Dodoma na Dk. Phillip Mpango, wakati akisoma taarifa ya hali ya uchumi kwa mwaka 2018 na mpango wa maendeleo wa taifa wa mwaka 2019/20.

 “Ongezeko la wastani  wa asilimia 5.6, kiasi hicho ni sawa na dola 1,090 ikilinganishshwa na dola 1,044 kwa mwaka 2017 ambayo ni  sawa na ongezeko la asilimia 4.4,” amesema Dk. Mpango.

Akitoa taarifa hiyo Dk. Mpango amesema, pato la Taifa kwa mwaka 2018, limekuwa kwa wastani wa kiwango cha asilimia 7.0, ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.8 mwaka 2017.

Dk. Mpango ameeleza sababu za ukuaji huo, ikiwemo kuongezeka kwa uwekezaji hususan miundombinu ya ujenzi barabara, reli, viwanja vya ndege, kutengemaa kwa upatikanaji nishati ya umeme, kuimarika kwa huduma za usafirishaji na hali nzuri ya hewa iliyopelekea uzalishaji mzuri wa chakula.

“Mwaka 2018 serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu, ilifanya maboresho ya takwimu za pato la taifa kwa kutumia mwaka 2015 kama mwaka wa kizio kutoka mwaka 2007, kufuatia marekebisho hayo mabadiliko kadhaa yalijitokeza ikiwa pamoja na mfumo, ukubwa wa pato la taifa, viwango vya ukuaji pato la taifa kisekta na uwiano wa viashiria mabalimbali kwa pato la taifa,” amesema Dk. Mpango na kuongeza:

“Kwa mujibu wa takwimu mpya ya mwaka wa kizio wa 2015, pato halisi lilikuwa kwa kiwango cha asilimia 7.0 mwaka 2018 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.8 mwaka 2017.”

Dk. Mpango amezitaja sekta zilizotoa mchango mkubwa katika ukuaji wa pato la taifa, ikiwemo sekta ya kilimo iliyochangia kwa asilimia 28.2, ujenzi asilimia 13.0 na biashara na matengenezo asilimia 9.1.

Aidha, Dk. Mpango ametaja shughuli za kiuchumi zilizokuwa kwa kasi kubwa, ikiongozwa na sekta ya sanaa na burudani iliyokuwa kwa asilimia 12.7, ujenzi asilimia 12.9, uchukuzi na uhifadhi wa mizigo asilimia 11.8, sekta ya kitaaluma, sayansi  na ufundi asilimia 9.9, habari na mawasiliano 9.1 pamoja na kilimo asilimia 5.3.

Kwa upande wa mfumuko wa bei wa taifa, Dk. Mpango amesema mfumuko huo kwa mwaka 2018 uliendelea kubaki kwa wigo wa tarakimu 1 baada ya kupungua kutoka asilimia 5.3 mwaka 2017 hadi asilimia 3.5 mwaka 2018.

Hata hivyo, amesema katika kipindi hadi kufikia mwezi Aprili 2019, mfumuko wa bei ulifikia 3.2 ukilinganisha na asilimia 3.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2018.

“Kiwango hiki  kilitokana na sababu za kuimarika hali ya upatikanaji chakula katika katika masoko ya ndani na nchi jirani,  uzalishaji wa chakula nchini uliofikia tani mil 15.9 ikilinganishwa na mahitaji ya tani mil 13.3 na kuwa na utoshshelezi wa chakula kw awastani wa asilimia 124,” amesema Dk. Mpango.

Kuhusu thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma za nje ya nchi katika kipindi cha mwezi Julai hadi Aprili 2019, Dk. Mpango amesema ilifikia ilifikia dola za Marekani bil 7.2 ikilinganishwa na dola bil 7.29 mwaka 2017/18 kipindi kama hicho.

Vile vile, Dk. Mpango amesema akiba ya fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kuridhisha na kuendelea kukidhi mahitaji ya kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi na pia kuongeza imani ya wawekezaji katika uchumi, kutokana na kufikia dola bil 4.39 mwezi Aprili 2019.

Dk. Mpango amesema kiasi kinatosha kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi cha takribani miezi  4.3 ikiwa ni zaidi ya lengo la nchi la kuwa na akiba ya kutosha ya kuagiza bidhaa nje ya nchi kwa muda wa miezi 4.0.

Hali kadhalika, Dk. Mpango amesema mwenendo wa thamani ya shilingi  imeendelea kuwa imara ambapo katika kipindi cha kuishia mwezi Aprili 2019 dola 1 ilibadilishwa Sh. 2300.9 ikilinganishwa na Sh. 2270.3 katika kipindi kama hicho mwaka 2018.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!