Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Lwaitama amchambua Magufuli, Lissu
Habari za Siasa

Dk. Lwaitama amchambua Magufuli, Lissu

Dk. Azaveli Lwaitama
Spread the love

WAGOMBEA wawili kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, wana mambo mazito ya kushawishi wananchi hivyo kufanya uchaguzi kuwa mgumu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Dk. Azaveli Lwaitama, Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wakati akihojiwa na MwanaHALISI TV.

Dk. Lwaitama amewataja wagombea hao kuwa ni Dk. John Magufuli, mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Tundu Lissu, Mgombewa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Amesema Dk. Magufuli, Rais anayemaliza muda wake, amejipambanua katika uongozi wake kama mchapakazi na aliyejikita katika utekelezwaji wa miradi inayoonekana hasa ya miundombinu ya barabara na madaraja.

Hivyo, anaweza kupata kura za Watanzania wanaopenda maendeleo ya vitu, wakati Lissu anaweza kupata kura za huruma kufuatia tukio lake la kushambuliwa na risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma tarehe 7 Septemba 2017.

“Uchaguzi huu ni mgumu na una sura mbili, moja wako watu nina uhakika wanasema Rais huyu andelee, nina uhakika wako wa kutosha, kitakachosema ni nini itatokana na uchaguzi kuwa huru na haki.”

“Nina uhakika mgombea wa chama tawala ana nafasi ya kupata watu wa kuunga mkono, wanaosema anajitoa muhanga haya anayofanya hayawezi kuwa na faida sasa hivi. Baadaye yatasaidia, lakini itategemea hawa wapiga kura milioni 29 wangapi walioathirika hasi na walioathirika chanya na hii ndio maana ya uchaguzi duniani,” amesema Dk. Lwaitama.

Akielezea sura ya uchaguzi huo, Dk. Lwaitama amesema, utakuwa uchaguzi wa maendeleo ya vitu na uhuru wa watu, kutokana na Tanzania ilivyoendeshwa kwa muda wa miaka mitano.

John Magufuli, Mgombea Urais na Mgombea mwenza wake, Samia Suluhu wakirudisha fomu za kugombea urais

“Kama mchambuzi, nafikiri kuna mambo mawili ya kuangaliwa, moja kwa kipindi miaka mitano chama kilicho madarakani kimetengeza mazingira ya kufanya siasa peke yake, kilikuwa kinazungumza halafu serikali yake inafanya mambo makubwa makubwa yanayoonekana ambayo inaweza kutumia katika kujinadi.

“Hasa miundombinu inaweza kutumika vizuri kwenye kampeni, lakini kiongozi wake alivyokuwa anaongoza serikali kutumbua na kujibu matatizo ya watu. Ana nafasi ya kupata kura za kutosha sababu kuna watu wengine wataangalia madaraja, ndege na reli,” amesema Dk. Lwaitama.

Akimzungumzia Lissu amesema, Lissu anaweza kusimama na kuwaeleza wananchi kuwa ‘akisimama hivi kitu cha kwanza anasema nimeumia sana.”

Amesema, Chadema na mgombea wake wanaweza kutengeneza hisia katika kipindi kifupi ikafunika kabisa ile faida (nafasi ya chama tawala ya miaka mitano iliyopita).

Tundu Lissu-Chadema

“Ni mtu ambaye anayeweza kutengeneza hisia kali kwa kipindi kifupi. Historia inaonesha vyama ama makundi yaliyowahi kuzuiliwa, yakiwa na mtu ambaye anaweza kutengeneza hisia kali kwa wananchi, yanaweza kufunika faida za chama kingine kufanya peke yako mikutano kwa miaka mitano,”

Akizungumzia muungano wa vyama vya upinzani Dk. Lwaitama amesema, kama vyama hivyo vinataka kupata mafanikio hususan katika uchaguzi wa wabunge na madiwani, vinapaswa kuacha ubinafsi.

“Ushauri wangu itakua ni kwamba hivyo viburi ndani ya vyama kufikiria ruzuku msiposhirikiana mtakosa hiyo ruzuku. Mpime kwamba huyu atafanikiwa hapa, hapa huyu ataweza, kiwango watakachoelewana ndipo watashinda,” amesema Dk. Lwaitama.

Kwenye uchaguzi wa Urais wa Tanzania, amesema hata kama wasipoungana haitaleta athari kubwa kwao kwa kuwa hakuna mgombea wa vyama vya upinzani atakayeweza kupunguza kura za mgombea wa Chadema, kwa maelezo kwamba mgombea wa chama hicho ana ushawishi mkubwa.

Bernard Membe-ACT-Wazalendo

“Kwenye ngazi ya urais ni tofauti kidogo,  sababu ngazi ya urais tumeona kwenye historia, hata wakati wa kupigania uhuru vyama vikilikuwa vingi laki ni Tanu kiliibuka, unaweza kufikiria watu utawachanganya kwa kuwa na wagombea wengi lakini wakamchagua yule wanayemtaka,” amesema Dk. Lwaitama.

Dk. Lwaitama amesema, “hata ukitafuta kuwachanganya wapiga kura kwa kuweka wagombea wengi sidhani, mfano Tanzania hii wagombea wanaoonekana na ushawishi ni wa Chadema au ACT-Wazalendo, kama  watakuwa wamepitishwa na tume wao wanajua ni nani kati yao wana mvuto.

Hata wakijichanganya bado hawajashirikia huyu aliyetoka CCM itapunguza kura za CCM kuliko kura za Chadema, yaani huyu aliyehamia ACT juzi ana mvuto wa kupunguza kura za mgombea wa Chadema bali  ana nguvu za kupunguza kura za CCM za watu alioondoka nao.”

2 Comments

  • Msidanganyike watnzania wenzangu “amani Kwanza” hakuna mtawala ataye gawa pesa bila sisi wenyewe kujituma kufanya kazi wapinzani Wana njaa na kiu ya utawala watatupeleka pabaya hawana focus nzuri watagawana nchi Kisha tutamkumbuka”jpm”many votes to JPM

  • Hakuna sababu ya upendeleo tz kwani nchi ni yetu site..na hakuna wa kuiuza wala kuleta vita jeshi lipo halina chama.Nchi yetu inaendeshwa kwa sheria kwa hiyo hakuna wa kugawana ardhi ya tz tuache danganya watu bure.Mgombea yeyote km anapita ni haki yake nchi hakijaumbiwa chama kimoja Bali watz wote kwani wagombea wanatokea nje ya nchi?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!