February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Kalemani aipa maagizo TANESCO

Dk. Medard Kalemani, Waziri wa Nishati

Spread the love

WAZIRI wa Nishati, Dk. Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme wa Ugavi nchini (TANESCO), kuhakikisha umeme haukatiki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Pia amelitaka shirika hilo kutoa taarifa pale linapolazimika kukata umeme kwa sababu za msingi na kuurejeshwa kwa haraka.

“Pale mnapolazimika kukata umeme kwa sababu za msingi, itolewe taarifa,” amesema Dk. Kalemani na kuongeza “..na umeme urejeshwe muda ulioandikwa kwenye taarifa hiyo.”

Dk. Kalemani ametoa maagizo hayo wakati alipokutana na wakuu wa Taasisi na Menejimenti za Wizara ya Nishati, jijini Dodoma.

Waziri huyo amezitaka taasisi hizo kuhakikisha miradi inayosimamiwa na wizara hiyo inakamilika kwa wakati.

Pia amesema, licha ya kukamilika kwa wakati anataka kuona miradi hiyo inakamilika kwa ubora ulinaokubalika na si vinginevyo.

error: Content is protected !!