Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Bashiru: Wabunge kujivua uanachama ni faida kwa Upinzani
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Bashiru: Wabunge kujivua uanachama ni faida kwa Upinzani

Spread the love

DK. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM amesema kitendo cha wabunge na madiwani wa vyama vya CUF na Chadema kujivua unachama na kujiunga na chama chake, ni faida kwa vyama hivyo vya upinzani. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea)

Dk. Bashiru ameyasema hayo leo tarehe 15 Agosti, 2018 wakati akihojiwa na kituo kimoja cha luninga kuhusu hasara iliyongia Taifa katika kuitisha uchaguzi mdogo kufuatia uamuzi wa wabunge hao kujivua ubunge.

Ameeleza kuwa, sababu zinazotolewa na wabunge hao pindi wanapohama ni ujumbe tosha kwa vyama vya upinzani wanakotoka, utakaowasaidia kujitathimini kama wako sahihi au la!.

“Ndiyo mfumo uliopo ni kwamba mtu akitoka kwenye chama baada ya kuridhika kwamba chama hakifai na hakifuati misingi niliyoifuata sina sababu ya kuwa mtumwa, na akiamua kuondoka utaratibu unasema amepoteza kila kitu…Ndiyo tiba ninayosema, kuna hasara ya kifedha lakini kuna faida ya kutibu majeraha kwenye mfumo wa kisiasa kwanza,” amesema Dk. Bashiru na kuongeza.

“Ni ishara ya kutuma ujumbe kwa vyama kwamba mkianza kubinafsisha vyama watu watawakimbia, badala ya kukaa na vyama vinavyowachonganisha vinavyoodhofisha mchakato wa kisiasa na mfumo wa kidemokrasia hiyo nayo gharama inaweza kuwa halali, gharama ya kujitathimini kama taifa na vyama vyenyewe kujitathimini pengine ingekuwa vigumu kwa vyama vyenyewe kujijua kama viko sahihi au haviko sahihi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!