Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM

Dk. Bashiru: CCM itaongoza zaidi ya miaka 100 ijayo

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally amesema kuwa, chama hicho kitaendelea kuongoza dola kwa zaidi ya miaka 100 ijayo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza kwenye ziara yake mkoani Mwanza leo tarehe 22 Mei 2019, katibu huyo amesema, CCM ina misingi iliyo imara inayokiwezesha kuendelea kuwepo madarakani.

Dk. Bashiru yupo ziarani Mwanza kukagua miradi ya CCM ambapo amesema, chama hicho hakiwezi kuondolewa madarakani kwa kuchagizwa na mijadala ya mitandaoni.

“Kuiondoa CCM madarakani kunahitaji kuwa na mkia mrefu,” amesema Dk. Bashiru akisisitiza kuwa, kura zinapigwa na wananchi na sio mitandaoni.

Dk. Bashiru amesema kuwa, fikra sahihi kwa wanachama, uhuru na usawa ndio nguzo muhimu inayokiwezesha chama hicho kuendelea kuwa na ndoto ya kutawala dola kwa zaidi ya miaka 100 ijayo.

 “Serikali ambayo inahakikisha inalinda rasilimali, haipangiwi cha kufanya, kulinda uhuru sambamba na kuwekeza kwa wananchi, itakuwepo kwa muda mrefu,” amesema.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally amesema kuwa, chama hicho kitaendelea kuongoza dola kwa zaidi ya miaka 100 ijayo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Akizungumza kwenye ziara yake mkoani Mwanza leo tarehe 22 Mei 2019, katibu huyo amesema, CCM ina misingi iliyo imara inayokiwezesha kuendelea kuwepo madarakani. Dk. Bashiru yupo ziarani Mwanza kukagua miradi ya CCM ambapo amesema, chama hicho hakiwezi kuondolewa madarakani kwa kuchagizwa na mijadala ya mitandaoni. “Kuiondoa CCM madarakani kunahitaji kuwa na mkia mrefu,” amesema Dk. Bashiru akisisitiza kuwa, kura zinapigwa na wananchi na sio mitandaoni. Dk. Bashiru amesema kuwa, fikra sahihi kwa wanachama,…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram