Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Bashiru amtisha Membe
Habari za Siasa

Dk. Bashiru amtisha Membe

Spread the love

SIKU mbili baada ya Bernald Membe kusema, uamuzi wa kumkabili Dk. John Magufuli kwenye urais ndani ya chama hicho, ndio uliomfukuzisha, Dk. Bashiru Ally amemtaka wakutane uwanjani. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Dk. Bashiru ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema ikiwa sababu alizozitoa Membe ndio kilichomfukuzisha kwenye chama hicho, basi ahamie kwenye vyama vingine ili wakutane kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Dk. Bashiru anapingana na hoja ya Membe, kuwa kilichomponza ndani ya chama hicho si hatua zake kuelekea urais, bali utovu wa nidhamu usiovumilika.

Membe alitaka ‘kukomesha’ utamaduni wa CCM kwamba, rais aliyepo madarakani agombee muhula wa pili kupitia chama hicho.

Wiki iliyopita, Membe ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Mbunge wa Mtama, alilieleza gazeti moja la kila siku, kwamba hatua zilizochukuliwa na CCM, zilitokana na kuonesha dhamira ya kumkabili Dk. Magufuli, mwenyekiti wa sasa wa chama hicho katika hatua za kuteuliwa kugombea urais kupitia chama hicho.

Leo tarehe 2 Machi 2020, akiwa katika ofisi za Mwananchi Communication, Dk. Bashiru amemueleza Membe kwamba, Katiba ya CCM haiifungi Katiba ya nchi, na kwamba anaruhusiwa kugombea urais kupitia chama kingine.

“Ukifukuzwa CCM, Katiba haisemi usigombee kwenye vyama 19 vingine,” amesema Dk. Bashiru na kuongeza “ila ukifungwa ndio unaweza ukakosa sifa au ukikwepa kodi, adhabu aliyopewa haihusu sharia za nchi.”

Membe na makatibu wakuu wastaafu wa chama hicho – Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba – waliingia matatani baada ya sauti zao kunaswa zikidaiwa kukejeli uongozi wa chama hicho chini ya Dk. Magufuli

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!