Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Bashiru alia wapinzani kuiumiza CCM
Habari za Siasa

Dk. Bashiru alia wapinzani kuiumiza CCM

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally amelalamikia vyama vya upinzani kukichafua chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, kampeni za mwaka huu kuelekea uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, zina viashiria visivyo vya kawaida na kwamba, mgombea wa chama chake Dk. John Magufuli ndio mlengwa mkuu wa kuchafuliwa.

Akizungumza kwenye kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Habari cha ITV cha tarehe 14 Septemba 2020, amedai baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani hawajajiandaa.

Amesema, wanasiasa hao hawajajiandaa kufanya kampeni kwa hoja, badala yake wameamua kuchukua uamuzi wa kuichafua CCM na mgombea wake.

“Unajua kampeni za mwaka huu kidogo zina viashiria visivyo vya kawaida kisiasa, kwa maana baadhi ya wanasiasa nadhani hawajajiandaa kufanya kampeni kwa hoja.

“Wameamua kuchukua uamuzi wa kutuchafua na mlengwa mkubwa ni mgombea wetu wa Urais,” amesema Dk. Bashiru.

Dk. Bashiru ametoa wito kwa wanasiasa kutumia mikutano ya kampeni kujibizana kwa hoja, si kuchafua historia ya CCM kwa kuwa wakiendelea, chama hicho hakitanyamaza kimya.

“Sasa wakitokea wanasiasa ambao wanataka kututoa katika misingi hiyo ambayo kwa kweli ni utamaduni mpya, CCM haiwezi ikanyamaza na kwa sababu tuko wengi, nikianza kuwafungulia hao watu wajibu watapotea tu,” amesema Dk. Bashiru.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

error: Content is protected !!