Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Bashiru aeleza namna dola inavyoibeba CCM
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Bashiru aeleza namna dola inavyoibeba CCM

Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM
Spread the love

WAKATI Rais John Magufuli akiahidi uchaguzi huru na haki, Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), anashangazwa namna vyama vilivyo madarakana kushindwa kuendelea kubaki madarakani kwakutumia dola. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, chama kilichopo madarakani kikishindwa kutumia dola kubaki madarakani, huo unakuwa uzembe wao, akitolea mfano wa uzembe uliofanywa na Chama cha KANU cha nchini Kenya na Unip cha Msumbiji.

Akizungumza na Kampuni ya Habari ya IPP leo tarehe 6 Machi 2020, Dk. Bashiru amesema, vyama hivyo (KANU na Unio) vilishindwa kutumia afueni ya dola iliyokuwa mikononi mwao kubaki madarakani, ndio maana vilianguka.

Amehoji, chama kinawezaje kushika dola kisha akatokea mwenye busara kutaka kutotumia dola, na kwamba pale kitapoondolewa madarakani, hakiwezi kurudi.

“Unashika dola halafu unatumia dola kubaki kwenye dola, halafu akitokea mtu ambaye ana busara zaidi kukwambia usitumie dola kubaki kwenye dola ukamsikiliza, siku ukishatoka hurudi,” amesema Dk. Bashiru.

Akionesha kuwa huo ndio mtindo wa ‘vyama dola’ Afrika, Dk. Bashiri ameeleza, kwamba vyama vya upinzani ikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha ACT-Wazalendo, kwamba vikichukua madaraka navyo vitatumia dola kubaki madarakani.

Hata hivyo, amesema dola hiyo haipaswi kutumika kunyanyasa washindani wa vyama vingine.

“…Hata Chadema ikiingia kwenye dola, kuiondoa kwenye dola itakua ni uzembe wake kwa sababu ana nafuu na faida kuwa na dola,” amesema Dk. Bashiru na kuongeza “kinachotakiwa usitumie dola vibaya kunyanyasa washindani wako.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!