Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Bashiru: Wapuuzeni hao wapumbavu
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Bashiru: Wapuuzeni hao wapumbavu

Spread the love

LUGHA kali na zenye ukakasi, zimeanza kutolewa na viongozi wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), juu ya barua iliyoandikwa na viongozi wastaafu wa chama hicho. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM ametumia neno ‘wapumba’ wakati akipongeza hatua ya wanaCCM Mkoa wa Dodoma, kutaka Kanal Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba, makatibu wastaafu wa CCM kuchukuliwa hatua.

Ni baada ya makatibu hao wastaafu wiki iliyopita, kumwandikia barua Pius Msekwa, Katibu wa Baraza la Viongozi Wastaafu wa CCM wakilalamikia kuchafuliwa na Cryspian Musiba, anayejitambulisha kuwa mtetezi wa Rais John Magufuli.

Kwenye barua hiyo, Makamba na Kinana wamelalamika kuchafuliwa na kuzushiwa huku serikali ikishindwa kuchukua hatua. Hata hivyo, wamehoji ‘ulinzi’ anaopewa Musiba.

Akizungumza tamko lililotolewa na Halmashauri ya CCM Mkoa wa Dodoma jana, Dk. Bashiri amewataka makada wa chama hicho kuwapuuza ‘wapumbavu’ hao.

“Wapuuzeni hao wapumbavu, hatuogopi kukosolewa, lakini hatuko tayari kudharauliwa, kutukanwa na kubezwa na majina yaliyo na kebehi na watu wasio na shukrani. Hatujafunzwa hivyo, hatujazoea hivyo,” amesema Dk. Bashiri bila kutaja jina lolote.

Akizungumzia tamko hilo leo tarehe 23 Julai 2019 Dodoma, Dk. Bashiru ameonya wanachama wa CCM watakaoendeleza mjadala ndani ya chama hicho, ili kujipatia umaarufu wa kisiasa. Amesema, wakibainika watachukuliwa hatua.

 “Kuna watu wanasema kwamba CCM imetumbuka na kutumbuliwa na kila aina ya kejeli. Kwa kweli Kiswahili chepesi nilichosema wapuuzeni hao wapumbavu, na ole wake mwana CCM abainike nanafanya malumbano ya kireja reja, atachukuliwa hatua,” amesema.

Aidha, Dk. Bashiru amesema, uongozi wa CCM hautaruhusu malumbano ndani ya chama hicho, huku akieleza kwamba mwenyekiti wake, Dk. Magufuli yuko tayari kuwasamehe, ili kukijenga chama.

“Msijifanye majasiri wa kupambana na malumbano, hakuna ruksa hiyo kwenye chama chetu. Waacheni wabwabwaje kitoto toto watachoka wenyewe.

“…ole wake mwanaCCM yeyote atakayetaka kutumia fursa ya upumbavu wa wapumvavu wa mwaka kutafuta kiki, ya kisisasa ili achaguliwe kwenye seriali za mtaa, hapana msifanye hivyo,” amesema Dk. Bashiru.

Mbele ya wanaCCM hao amesema, “Jifunzeni kutoka kwa kiongozi wetu ambaye wakati wote hana muda wa malumbano. Amevumilia, wanaomtusi wengine wana umri wa watoto wake amewavumilia na yuko tayari kuwasamehe pia.  Lakini kwa kufanya hivyo si kwamba ni muoga.”

Dk. Bashiru amesema, chama hicho hakikatazi kukosolewa, lakini kina utaratibu wa kukosoa kistaarabu.

“Mwalimu Julius Nyerere alishatuhasa tujisahihishe, kujisahihisha ni kujiimarisha, tujikosoe, tukosoane kwa adabu kwa nidhamu tuache utoto. Kisiwe chama cha siasa za kipuuzi, sababu majira haya ni ya uchaguzi,” amesema Dk. Bashiru.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!