Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Diwani ataka ushirikiano ili kukuza elimu
Elimu

Diwani ataka ushirikiano ili kukuza elimu

Wanafunzi
Spread the love

DIWANI wa Kata ya Ipagala Gombo Dotto (CCM) amewataka viongozi wa kata hiyo, wazazi na walimu kushirikiana kwa ukaribu ili kuwezesha watoto wao kupata elimu bora. Anaripoti Danson Kaijage… (endelea)

Gombo alitoa kauli hiyo hivi karibuni katika kikao cha wazazi, walimu na watendaji wa serikali wa kata ya Ipagala iliyopo Jijini Dodoma wakati wa kufanya tathimini ya matokeo ya kidato cha nne na cha pili katika shule ya sekondari ya Makole.

Katika tathimini hiyo shule ya sekondari Makole katika matokeo ya kidato cha nne imeweza kushika nafasi ya 18 kimkoa kati ya shule 117 na kufanikisha kufikia kiwango cha ufahuru kwa asilimia 93.1 na kitaifa imeshika nafasi ya 837 kati ya shule 3488.

Diwani huyo alisema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika shule za kata lakini bado wazazi hawajawa na mwamko mkubwa wa kushirikiana na walimu ili kuweza kubaini yapo mapungufu gani kati ya mwalimu na mwanafunzi.

Akizungumzia shule ya sekondari ya Makole Gombo alisema kuwa kwa matokeo ya kidato cha pili na kidato cha Nne kwa mwaka 2018 shule hiyo imeweza kufanya vizuri baada ya bodi ya shule kuweka mikakati ya ushirikiano kati ya bodi ya shule,wazazi, walimu na wanafunzi.

Diwani huyo alisema pamoja na shule ya sekondari Makole kufanya vizuri na kushika nafasi ya 18 kimkoa bado juhudi za makusudi zinahitajika kwa ajili ya kutafuta kumi bora au kushika nafasi ya kwanza kimkoa na kuingia kumi bora kitaifa.

Aidha alisema ili kuwapamotisha walimu ameahidi kupeleka sukari mfuko mmoja wenye kilo 25 shuleni hapo kila mwezi ili walimu waweze kupata chai wawapo shuleni hapo badala ya kutafuta chai katika vibanda.

Kwa upande wa mwalimu mkuu wa shule ya Makole Bonifas Chipana alisema kuwa siri ya shule hiyo kuweza kufanya vizuri mitihani kidato cha pili na cha nne ni ushirikiano kati ya walimu na wanafunzi sambamba na kuwafanya wanafunzi kuwa na nidhamu.

Aidha mwalimu huyo alisema kwa mikakati ya pamoja walimu walikubaliana kuwapa wanafunzi mitihani ya mara kwa mara ili kuwajengea uwezo wanafunzi wa kujisomea na kutokuwa waonga wa kufanya mitihani pale inapoletwa.

Alibainisha kuwa katika mikakati hiyo wanafunzi wote kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne wamekuwa wanafanya mitihani kabla ya kuanza vipindi saa mbili kamili huku wale wa kidato cha nne na pili wakiwa na muda wa ziada katika kupatiwa masomo zaidi na walimu.

Hata hivyo alisema licha ya kuwepo na sera ya Elimu bure bado kuna changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na wanafunzi kuongezeka mashuleni na kueleza kuwa fedha za kutoa machapisho kwa ajili ya mitihani ya majaribio kwa watoto kutokutosha.

Mkuu huyo wa shule pia alitoa wito kwa wazazi kushirikiana na walimu kwa ukaribu ili kuweza kutoa michango ambayo shule na wazazi watakuwa wamekubariana kwa ajili ya uchapishaji wa mitihani ya majaribio kwa wanafunzi huku akiupongeza uongozi wa kata kwa kuwa karibu na shule.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

error: Content is protected !!