MSANII Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemgalagaza mzazi mwenzake, Mwanamitindo Hamisa Mabeto katika kesi ya madai aliyoifungua katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kudai matunzo ya mtoto Prince Abdul, anaandika Angel Willium.
Hakimu Devotha Kisoka wa Mahakama hiyo ametupilia mbali madai ya Mobeto katika kesi hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika.
Diamond aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto akidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi. Hoja ambayo ilipingwa na Mobeto.
Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine anaiomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond.
Mwanamitindo huyo pia anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi na alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.
Kupitia hati hiyo ya madai, Mobeto anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.
Diamond aliwasilisha hati ya majibu hayo kinzani akipinga maombi hayo ya Mobeto akidai gharama anazodai kulipwa kwa mwezi ya Tsh. 5 milioni kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.
Leave a comment