Diamond kutumbuiza Simba Day, viingilio hadharani

Spread the love

MSANII wa kimataifa kutoka Tanzania, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz atakuwa miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kilele cha tamasha la mabingwa wa soka wa ligi kuu ya nchi hiyo 2019/20, Simba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Tamasha hilo linalojulikana kama ‘Simba Day’ litahitimishwa Jumamosi tarehe 22 Agosti 2020 katika viwanja viwili vya mpira Uhuru na Mkapa vyote vya jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa Simba, Haji Manara akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumatano tarehe 19 Agosti 2020 amesema, katika tamasha hilo, kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii maarufu nchini.

“Kutakuwa na burudani itatolewa na Twanga Pepeta, TundaMan, Meja Kunta, Mwasiti na kipekee atakuwepo Diamond Platinumz. Litakuwa kama tamasha la mziki na MC wetu atakuwa Mpoki (Silvery Mujuni,” amesema Manara.

Manara amesema, kutokana na ukubwa na umuhimu wa tamasha hilo, viwanja viwili vitatumika ambapo uwanja wa Uhuru kutakuwa na televisheni kubwa zitakazofungwa ambapo wachezaji wote wa Simba, kabla ya kuingia uwanja wa Mkapa, watakwenda kuwasalimia mashabiki watakaokuwa katika uwanja huo.

Amesema, timu ya Vital’O ya Burundi itakayocheza na Simba saa 10:15 jioni, itawasili nchini Ijumaa tarehe 21 Agosti 2020 saa 5 asubuhi na jioini ya siku hiyo, timu zote zitafanya mazoezi kwa kupishana kwenye uwanja wa Mkapa.

“Tulipanga kucheza na timu ya Al Ahly (Misri) lakini changamoto ya corona imefanya jambo hilo kuwa gumu. Tunaamini Vital’O itatupa changamoto nzuri kwenye mchezo huo,” amesema Manara

Kuhusu viingilio, Manara amesema Uwanja wa Uhuru itakuwa Sh.2,000. Katika Uwanja wa Mkapa Mzunguko itakuwa Sh.7,000, VIP C Sh.20,00, VIP B Sh.30,000, VIP A Sh.40,000 na kutakuwa na tiketi maalum za Platinum Sh.150,000.

“Tunajiandaa, tumeshaanza mazoezi, wachezaji wachache hawajafika kuytokana na ratiba za ndege lakini kesho tutakuwa wote. Tuwaombe wenzetu waanze kuandika malalamiko mapema. Wao wanadhurura. Kikao kiko kamili, wenzetu bado wako mitaani, waambieni,” amesema Manara.

MSANII wa kimataifa kutoka Tanzania, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz atakuwa miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kilele cha tamasha la mabingwa wa soka wa ligi kuu ya nchi hiyo 2019/20, Simba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). Tamasha hilo linalojulikana kama ‘Simba Day’ litahitimishwa Jumamosi tarehe 22 Agosti 2020 katika viwanja viwili vya mpira Uhuru na Mkapa vyote vya jijini Dar es Salaam. Msemaji wa Simba, Haji Manara akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumatano tarehe 19 Agosti 2020 amesema, katika tamasha hilo, kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii maarufu nchini. “Kutakuwa na burudani…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Masalu Erasto

One comment

  1. NAWATAKIA MANDALIZI MEMA SIMBA KWENYE SIMBA DAY HAPO JUMAMOSI BY JASTIN KIBONA KUTOKA MKOANI SONGWE WILAYANI ILEJE KATA YA KALEMBO KITONGOJI CHA IPASA

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!