DC Katambi amsimamisha afisa  kitengo cha ardhi, aagiza uchunguzi

Spread the love

MKUU wa Wilaya (DC) ya Dodoma mjini nchini Tanzania, Patrobasi Katambi ametangaza kumsimamisha kazi, Hadson Magomba, afisa kitengo cha mipango miji katika Jiji hilo kwa kushindwa kutenda haki kwa wananchi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea)

Mbali na kusimamishwa kazi, ametoa siku saba kwa mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwini Kunambi kuunda tume huru maalum ya uchunguzi dhidi ya dhuruma ambayo amefanyiwa Mdala Anna Mazengo kwa kudhurumiwa viwanja vyake na kupewa mtu mwingine.

Katambi ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko yaliyotolewa na mdala Mazengo wakati wa mkutano wa hadhara aliouitisha kwa ajili ya kupokea malalamiko juu ya kudhurumiwa ardhi katika kata ya Ipagala katika Jiji la Dodoma.

Katika mkutano huo, mdala Anna ambaye ni mjane toka mwaka 1985 na mwenye watoto kumi huku watoto wawili wakiwa wametangulia mbele ya haki alisema aliporwa maeneo yake katika maeneo ya swaswa extation ekari sita.

Mdala Anna alisema, pamoja na kuwa na eneo kubwa lakini afisa kitengo cha mipango miji wa Jiji la Dodoma ambaye alimtaja kwa jina la Hadson Magomba,alimnyanyasa kwa kutompa eneo lake huku akishindwa kumpa haki take na kubadilisha matumizi na eneo hilo kuwapatia watu wengine.

“Mimi ni mjane tangu mwaka 1985 na mwenzangu aliniachia watoto kumi japo watoto wawili wameisha tangulia mbele ya haki, watoto waliobaki ninawatunza na nilikuwa na maeneo mbalimbali hasa maeneo ya swaswa zaidi ya heka sita,” amesema

“Cha kushangaza baadaye maeneo yangu yalitwaliwa na wakati yanatwaliwa nilikuwa na vielelezo vyote na nilijaribu kufuatilia lakini niliambulia vitisho na maneno ya kejeri na matusi.”

“Nilienda katika kitengo cha mipango miji ili kuweza kusikilizwa lakini matokeo yake niliambulia kurushiwa barua na kama mbwa na Hadson Magomba jambo ambalo nilishindwa kupata msaada,” alisema Mdala Anna.

Aidha Mdala Anna alisema kinachomshangaza ni kuona maeneo yake yaliyotwaliwa bila fidia anaona nyumba zikijengwa jambo ambalo alidhani labda ni nyumba za walimu jambo ambalo si kweli kumbe ni nyumba za watu binafsi.

Katambi alisema tume hiyo inatakiwa kuundwa na watumishi kutoka ofisi ya mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini.

MKUU wa Wilaya (DC) ya Dodoma mjini nchini Tanzania, Patrobasi Katambi ametangaza kumsimamisha kazi, Hadson Magomba, afisa kitengo cha mipango miji katika Jiji hilo kwa kushindwa kutenda haki kwa wananchi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea) Mbali na kusimamishwa kazi, ametoa siku saba kwa mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwini Kunambi kuunda tume huru maalum ya uchunguzi dhidi ya dhuruma ambayo amefanyiwa Mdala Anna Mazengo kwa kudhurumiwa viwanja vyake na kupewa mtu mwingine. Katambi ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko yaliyotolewa na mdala Mazengo wakati wa mkutano wa hadhara aliouitisha kwa ajili ya kupokea malalamiko juu ya kudhurumiwa ardhi katika kata…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Danson Kaijage

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!