Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa DC aeleza kilichomponza Nyalandu mpakani Namanga
Habari za SiasaTangulizi

DC aeleza kilichomponza Nyalandu mpakani Namanga

Mkuu wa Wilaya ya Longido (DC), Mkoa wa Arusha, Frank Mwaisumbe
Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Longido (DC), Mkoa wa Arusha, Frank Mwaisumbe, ametoa sababu zilizomfanya Lazaro Nyalandu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda Kati kushindwa kuvuka mpaka wa Namanga kwenda nchini Kenya. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam …(endelea).

Nyalandu ambaye alikuwa mgombea Ubunge wa Singida Kaskazini alikutana na zuio hilo kutoka kwa mamlaka za Serikali ya Tanzania juzi Jumamosi tarehe 7 Novemba 2020.

DC Mwaisumbe, akizungumza na MwanaHALISI Online leo Jumatatu tarehe 9 Novemba 2020 amesema “ilikuwa juzi ambapo yeye alikuwa anataka kuvuka mpaka wa Namanga kuelekea Kenya lakini hakuwa na nyaraka muhimu kama hati ya kusafiria na nyaraka zingine za afya zinazohitajika.”

Kingine kilichomkwamisha mwanasiasa huyo kuvuka amesema, “alikuwa ana gari anaitumia aliyotaka kuvuka nayo kwenda Kenya lakini haikuwa imesajiliwa kwa jina lake. Gari lilikuwa limeandikwa jina la mtu mwingine, lakini yeye alidai ni la kwake.”

“Kama unataka kuvuka na gari na huna nyaraka zinazoonyesha unamiliki lazima uwe na nyaraka zilizokamilika na tukamwambia aende akatimize nyaraka na mkataba wa gari hilo alilonunua na tulimweleza aje leo lakini hadi sasa (ilikuwa saa 10 jioni) hajaja,” amesema Mwaisumbe.

Zuio hilo la Nyalandu aliyewahi kuwa waziri wa maliasili na utalii katika utawala wa awamu ya nne wa Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, limetokea kipindi ambacho kumekuwa na wimbo la wanasiasa wa upinzani kuondoka nchini kwa ajili ya kutafuta hifadhi.

Godbless Lema, aliyekuwa mgombea ubunge wa Arusha Mjini, anashikiliwa na mamlaka za Kenya akidaiwa kuingia nchini humo bila kufuata taratibu.

Lema amekimbilia nchini Kenya, ili kuomba hifadhi ya kisiasa, katika ubalozi wa Marekani, jijini Nairobi.

Hayo yakiwasibu hao, aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema, Tundu Lissu anaendelea kuishi nyumbani kwa Balozi wa Ujerumani alipokwenda kuomba hifadhi akihofia ‘usalama wake.’

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

error: Content is protected !!