Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Dawasa yawafikisha kortini wadaiwa sugu
Habari Mchanganyiko

Dawasa yawafikisha kortini wadaiwa sugu

Afisa Sheria wa Dawasa, Omary Kipingu (katikati) akiwa na wafanyakazi wenzake wa mamlaka hiyo nje ya Mahakama ya Mwanzo Ilala
Spread the love

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) nchini Tanzania, imeanza kuwachukulia hatua za kisheria wateja wake wanaoshindwa kulipa bili za maji kwa kuwafikisha mahakamani wadaiwa sugu wakidaiwa Sh.8.01 milioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ilaka … (endelea).

Waliopandishwa katika Mahakama ya Mwanzo Ilala jijini Dar es Salaam jana Jumanne tarehe 1 Septemba 2020 na deni analodaiwa ni; David Mgaya (Tabata) Sh. 1.08 milioni na Ahad Gurisha mkazi wa Kisukuru Tabata Sh.2.95 milioni aliyepunguza Sh.400,000.

Wengine ni; Tune Juma mkazi wa Kibangu Ubungo anayedaiwa Sh.584,707, Rahima Sarakikya mkazi wa Buguruni anayedaiwa Sh.742,857, Hassan Khamis mkazi wa Buguruni Mnyamani Sh.733,008, Zacharia Okoth mkazi wa Tabata Sh.592,964 na Ashura Embe mkazi wa Buguruni Mnyamani Sh.1.31 milioni.

Washitakiwa hao walipandishwa kizimbani mbele ya mahakimu wawili tofauti na waliofika mahakamani ni Gurisha na Juma huku wengine watano hawakufika licha ya kupewa wito wa kuhudhuria mahakamani.

Gurisha na Juma baada ya kusomewa makosa yao na Afisa wa Sheria Dawasa, Omary Kipingu mahakamani hapo ambapo walikubali ni kweli wanadaiwa.

Bomba la maji safi

Hivyo walikubali kuingia mkataba wa makubaliano wa kulipa deni hilo hadi liishe ambapo mshatakiwa Gurisha alikubali kulipa Sh.320,000 kila tarehe 28 ya mwezi kwa miezi sita aliahidi kumaliza deni hilo ifikapo tarehe 28 Aprili 2021.

Naye Juma aliyeingia makubaliano ya kulipa deni hilo ni Mama mwenye nyumba wake, naye Gregory Kahwili ambaye alihaidi kuwa ifikapo tarehe 30, Septemba 2020 atalipa Sh.200,000 ambapo deni lililobaki atalipia kila mwezi Sh.100,000 litakamilika  30 Januari, 2021.

Hata hivyo, Mahakama hiyo ilitoa agizo la mwisho kwa wadaiwa hao kufika Mahakamani hapo ambapo imetoa hati ya wito kwa wadaiwa watatakiwa kufika tarehe 11 Septemba, 2020 mahamakani hapo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!