Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Dawasa yaibuka na mikakati lukuki Dar
Habari Mchanganyiko

Dawasa yaibuka na mikakati lukuki Dar

Spread the love

MAMLAKA ya Maji Safi na Taka Jijini Dar es Salaam (DAWASA), imetangaza mkakati mpya wa kukarabati miundombinu yake ikiwamo mabomba yaliyotoboka, anaandika Irene David.

Hayo yamesemwa na Romanus Mwang’ingo, Kaimu Mkurugenzi Dawasa, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO), Jijini Dar es Salaam.

Amesema Dawasa imeanza kutekeleza miradi mbalimbali inayolenga kuongeza upatikanaji wa maji, kusambaza maji katika maeneo mbalimbali, kukusanya na kusafirisha maji taka.

Mwang’ingo amesema moja ya miradi wanayotarajia kuishughulikia ni pamoja na upanuzi wa mtambo wa maji wa Ruvu chini kutoka uzalishaji wa maji mita za ujazo 180,000 hadi 270,000, ulazaji wa bomba kuu la mita 1.8 kutoka Ruvu chini hadi matenki ya chuo kikuu cha Ardhi na ujenzi wa ofisi za kuendeshea mradi huo.

Kwa upande wa mabomba yaliyotoboka kuyakarabati, Mwang’ingo amesema suala hilo lipo kwenye moja ya mikakati yao endelevu na hivyo wananchi wasihofu kwani litashughulikiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!