January 22, 2021

Uhuru hauna Mipaka

David Kameta asaini Simba

Spread the love

KLABU ya Simba imemsajiri aliyekuwa beki wa Lipuli FC, David Kameta, kwa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuimalisha kikosi chao kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajia kuanza 6, Septemba, 2020. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kameta amejiunga na Simba baada ya kuonesha kiwango bora kwenye michezo ya ligi kuu akiwa na kikosi cha Lipul kutoka mkoani Iringa ambayo kwa sasa imeshuka daraja.

Usajili wa mchezaji huyo umetangazwa leo kupitia mitandao yao ya kijamii ambayo toka jana imeanza kutambulisha wachezaji wapya watakaotumikia timu hiyo kwa msimu ujao.

Kusajiliwa kwa Kameta kutaenda kutia chachu kwenye eneo la ulinzi wa upande wa kulia ambao kwa sasa lipo chini ya Shomari Kapombe ambaye amekuwa kwenye kiwango bora toka aliporudi kwenye timu hiyo akitokea Azam FC.

Mpaka sasa klabu ya hiyo imeshasajili wachezaji wanne toka kufunguliwa na dirisha kubwa la usajili 1 Agosti, 2020 ambalo litadumu kwa kipindi cha mwezi mmoja tu.

Wachezaji wengine waliosajiliwa na klabu hiyo mpaka sasa ni Bernad Morrison kutoka Yanga, Joash Onyango kutoka Gor mahia,Charles Ilamfia aliyekuwa kmc na beki aliyekuwa anacheza Costal Union Ibrahim Ame.   

error: Content is protected !!