Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Daktari ataja njia zinazoambukiza Homa ya Ini
Afya

Daktari ataja njia zinazoambukiza Homa ya Ini

Dk. Crispin Kahesa, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kinga ya Saratani ya Ocean Road (ORCI)
Spread the love

KUHUSANA mwili wenye majimaji ikiwa ni pamoja na damu kutoka kwa mama (mwenye maambukizi) kwenda kwa mtoto wakati wa njia ya mama kujifungua kunachangia maambukizi ya virusi vya homa ya ini. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Pia kushirikiana vitu vyenye ncha kali kama sindano, viwembe na hususani wale wanaotumia dawa za kulevya, kujamiiana pasipo kutumia kondomu.

Hiyo ni kauli ya Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kinga ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dk. Crispin Andrew Kahesa akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 30 Julai 2019 jijini Dar es Salaam.

Pia amesema, watu 481 wamejitokeza kupima afya zao katika taasisi hiyo ili kutambua kama wameambukizwa virusi vya homa ya ini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 30 Julai 2019, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kinga ya taasisi hiyo, Dk. Crispin Andrew Kahesa amesema, idadi hiyo imeongezeka kutoka watu 150 ilivyokuwa awali (481).

Dk. Kahesa amezungumza kuhusu kambi maalum ya uchunguzi wa virusi vya homa ya ini bila malipo, iliyoanza kufanyika tarehe 27 Julai 2019ambayo itafika tamati taehe 31 Julai 2019.

Amesema, kambi hiyo imewekwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani ambayo kilele chake huwa huwa tarehe 28 Julai ya kila mwaka. Kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘Tafuta mamilioni ya watu wenye maambukizi ya homa ya ini’.

Amesema, kauli mbiu hiyo inalenga kila nchi kuhakikisha inawatambua watu wenye maambukizi ya homa hiyo, ili wapate matibabu na kuwapa chanjo wale wasio na maambukizi ili kuwakinga.

Dk. Kahesa amesema, kati ya watu wote 481 waliochunguzwa katika kampeni hii hadi sasa ni watu 18 wamekutwa na maambukizi.

“Mwitikio ni mkubwa kwa kundi la wanawake kuliko wanaume, nawasihi wanaume wenzangu nao wajitokeze kuchunguza, tumekusudia kuchunguza watu 1,000.

“Tangu mwaka 2018, ORCI ilipoanza kufanya uchunguzi na kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa huo, wameona watu wapatao 7,000 na 279 sawa na asilimia 3.9 kati yao walikutwa na maambukizi.

Amesema, hiyo inmaanisha katika kila watu 100 nchini, watu wanne wamepata maambukizi ya ugonjwa huu.

“Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaeleza kila mwaka watu wapatao milioni 10 duniani hugundulika kupata maambukizi kila mwaka,” amesema na kuongeza:

“Hii inamaanisha kwamba Watanzania wapo hatarini kupata maambukizi ya homa ya ini, virusi hivi vinaenezwa kwa njia mbalimbali hasa kupitia mfumo wa maisha.

Amesema, kugusana na majimaji ya mwili kama damu, kutoka kwa mama (mwenye maambukizi) kwenda kwa mtoto wakati wa njia ya mama kujifungua, kushirikiana vitu vyenye ncha kali kama sindano, viwembe na hususani wale wanaotumia dawa za kulevya, kujamiiana pasipo kutumia kondomu ni njia zinazoweza kusababisha maambukizi.

“Ndiyo maana tunatoa rai kwa jamii waje tuwafanyie uchunguzi ni vizuri kugundua mapema na kuanza tiba kuliko kuchelewa  wale ambao hawana maambukizo wahakikishe wana pata chanjo tatu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!