Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF (kushoto)

CUF yaiachia Chadema kata zote uchaguzi mdogo

CHAMA cha Wananchi CUF kimesema hakijasimamisha mgombea yoyote katika chaguzi za marudio zinazotarajiwa kufanyika Januari 22 mwakani katika kata 20, ananadika Pendo Omary.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo jioni Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF amesema hatua hiyo inatokana na mgogoro unaondelea ndani ya chama hicho.

Mgogoro unaoendelea ndani ya CUF ni juu ya Prof. Lipumba aliyejiuzulu uenyekiti wa chama hicho Agosti 2015 lakini Juni 2016 akatangaza kutengua uamuzi wake na kuirejea nafasi hiyo huku uongozi wa CUF chini ya Maalim Seif ukipinga na hatimaye kumvua uanachama lakini ameendelea kutambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa.

Mketo amesema hapo awali CUF ilikutana na vyama washirika katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) – Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NCCR – Mageuzi na National League For Democracy (NLD) ili kujadili namna vyama hivyo vitavyoshiriki katika uchaguzi ikiwemo kuachina kata.

“Sisi CUF tulikutana na vyama washirika wa ukawa katika kamati ndogo ya ufundi ya Ukawa ambapo tulikubaliana mambo kadhaa kuhusu kuachiana kata.

Wakati tukijiandaa kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa Ukawa katika uchaguzi wa marudio, ghafla akajitokeza Magdalena Sakaya (Mbunge wa Kaliua – CUF ambaye ni mfuasi wa Prof. Lipumba) na kutangaza kuwa CUF itasimamisha wagombea katika kata zote,” amesema Mketo.

Ameongeza kuwa, “Ieleweke kuwa hatujasimamisha wagombea sehemu yoyote na Sakaya na wenzake kutangaza kusimamisha wagombea katika kata zote ni utekelezaji wa kazi zao za kukisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupata ushindi.”

CHAMA cha Wananchi CUF kimesema hakijasimamisha mgombea yoyote katika chaguzi za marudio zinazotarajiwa kufanyika Januari 22 mwakani katika kata 20, ananadika Pendo Omary. Akizungumza na MwanaHALISI Online leo jioni Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF amesema hatua hiyo inatokana na mgogoro unaondelea ndani ya chama hicho. Mgogoro unaoendelea ndani ya CUF ni juu ya Prof. Lipumba aliyejiuzulu uenyekiti wa chama hicho Agosti 2015 lakini Juni 2016 akatangaza kutengua uamuzi wake na kuirejea nafasi hiyo huku uongozi wa CUF chini ya Maalim Seif ukipinga na hatimaye kumvua uanachama lakini ameendelea kutambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa. Mketo amesema hapo…

Review Overview

User Rating: 3.35 ( 2 votes)
0

About Pendo Omary

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube