Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CUF wakosoa kauli ya Maalim Seif
Habari za Siasa

CUF wakosoa kauli ya Maalim Seif

Mussa Haji Kombo, mgombea urais Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) (katikati) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani
Spread the love

KAULI ya Maalim Seif Sharif Hamad, mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo kwamba ‘vijana wawe tayari,’ imekosolewa vikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Mussa Haji Kombo, mgombea urais Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), amewataka wananchi kupuuza kauli hiyo akisisitiza kuwa, si mara ya kwanza wagombea wa upinzani kuwekewa pingamizi.

“Kauli zilizotolewa na Maalim Seif Sharif Hamad ni za hatari, zenye kushawishi vijana kuingia katika vurugu za kisiasa eti kwa sababu tu, wagombea wa chama chake wamewekewa pingamizi huko Pemba,” amesema.

Mgombea huyo ambaye leo Jumatano tarehe 2 Septemba 2020, anatarajiwa kuchukua fomu ya kugombea urais visiwani humo, ameeleza kwamba chama chao kitaingia kwenye uchaguzi huo kwa tahadhari ya kulinda amani.

Amesema, Wazanzibari hususani wakazi wa Pemba, bado wanakumbukumbu kwa yale yaliyowatokea mwaka 2001 baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2000.

Maalim Seif Sharrif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

“Wananchi Pemba hawajasahau watu waliopoteza maisha kwa sababu za vurugu za kisiasa mwaka 2001 na wengine kuwa wakimbizi Mombasa, Kenya,” amesema.

Amedai kwamba, sababu ya kutokea mauaji na ukimbizi mwaka huo, ni kutokana na Maalim Seif kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu.

Kombo ametoa wito kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini pamoja na mamlaka zingine kufanyia kazi kauli za Maalim Seif akidai, zikiachwa zinaweza kusababisha madhara.

Kuhusu chama hicho, Kombo amesema baadhi ya watu walikuwa wakidai kwamba kimesambaratika na kuwa ukweli wake, CUF bado ipo imara Zanzibar.

Hamida Abdallah, mgombea mwenza wa Kombo amewataka Wazanzibari kupuuza wito wa Maalim Seif kwa madai kuwa amekuwa mzee na akili yake imechoka.

Ijumaa tarehe 28 Agosti 2020, Maalim Seif alielezwa kukerwa na hatua ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaendgua wagombea wa upinzani hususan wa chama chake visiwani humo.

Alieleza kwamba, safari hii hatokubali na kuwataka wananchi kuwa tayari. Hata hivyo, hakueleza wawe tayari kwa lipi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema: Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!