Wednesday , 17 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CUF Lipumba watinga Dodoma
Habari za Siasa

CUF Lipumba watinga Dodoma

Spread the love

MBUNGE wa Mtwara Mjini, Mafutaa Nachuma (CUF) kwa kushirikiana na uongozi wa chama hicho mkoa wa Dodoma wamefungua ofisi ya mkoa mkoani Dodoma mtaa wa By Road. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Akizungumza na na waandishi wa habari, Kaibu wa CUF wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, Rajabu Mbalamwezi na mratibu wa shughuli zote za CUF mkoa wa Dodoma amesema kuwa ufunguzi wa ofisi hiyo ni kuhimalisha chama na kuweka mipango mikakati ya chama.

Mbalamwezi amesema kuwa kwa sasa umefika wakati wa kuondokana na makundi ndani ya chama hicho na kujenga chama kwa kutambua kuwa chama siyo cha mtu binafsi bali ni taasisi.

Amesema kuwa chama hicho kimekuwa na mgawanyiko wa pande mbili kwa maana ya kuwepo watu ambao wanamapinduzi ya Maalim Seif na wengine wamekuwa wakimwamini Prof. Lipumba.

Alisema makundi hayo kimsingi si ya wanachama bali ni ya wafuasi wa watu na kueleza kuwa mwanachama ambaye anatambua uanachama anazingatia zaidi kanuni,sheria na katiba ya chama.

Kwa upande wake ambaye anaamini kwa upande wa Profesa Lipumba amesema kuwa siyo kweli kuwa anaamini kwa Prof. Lipumba bali anaamini kwa mijibu wa katiba ya CUF na iwapo katiba ya chama hicho itamwondoa madarakani watafanya kazi na yule ambaye atakuwa kiongozi kwa mujibu wa katiba.

“Mimi na wanachama wengine ambao wanaamini na kuzingatia katiba ya chama hatupo upande wowote kwa maana ya upeneleo wa viongozi.

“Tunachoangalia ni katiba inasema nini kwa kuwa kwa sasa katiba inamtambua Prof.Ibrahim Lipumba basi inabidi kukubaliane na katiba iliyopo, na kama Maalim Seif angekuwa anatabuliwa na katiba tungeweza kufanya naaye kazi.

“Hiki chama siyo cha mtu bali ni taasisi hivyo wanachama wote watambue kuwa chama kinajengwa kwa misingi ya kuzingatia kanuni,sheria na katiba ya chama husika na wale wenye makundi siyo wanachana wa CUF bali ni wafuasi wa watu kwa mapenzi yao,” amesema Mbalamwezi.

Katka hatua nyingine Mbalamwezi amesema kuwa tangu wamefungua ofisi jijini Dodoma wamefanikiwa kupata wanachama wapya 486 huku akielezea kuwa kati ya hao wanachama 35 wametoka katika kata mtaa wa Chadulu kata ya Makole jijini Dodoma.

Aidha mbalamwezi amesema kuwa CUF imejipanga kuhakikisha inasmamisha mgombea kwenye kata zote 49 pamoja na kumsimamisha mgombea ubunge wa Jimbo la Buyungu kwa ajili ya kuziba nafasi iliyoachwa na aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo marehemu Mwalim Kaguku Bilago (Chadema).

Naye mkamu mwenyekiti wa CUF wilaya ya Dodoma Jiji, Ismail Seif, amesema kuwa kwa sasa ofisi hiyo ipo wazi na wanachama wanatakiwa kuitumia kwa manufaa ya chama hicho.

Aidha amesema kuwa kila mwanachama mwenye kuwa na maswali ya kuuliza ili kupata ufafanuzi juu ya chama hicho ni vyema akafika ofisi hapo.

“Ofisi hipo wazi wanachama wote wa CUF na wale wasiokuwa wanachama wanatakiwa kufika ofisini ili waweze kuuliza jambo lolote watajibikwa kwa misingi ya katiba ya chama pamoja na kanuni zake,” amesema Seif.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!