Picha zilizotolewa na Juve zimemuonyesha nyota huyo akifanya vipimo kabla ya kutambulishwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Allianz.
Juventus watalazimika kulipa pauni 50 milioni kwanza na kumalizia 50 zilizobaki mwisho wa mwaka kwa Real Madrid.
Mamia ya mashabiki wa Juventus wamejitokea kumpokea Ronaldo aliyewasili kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya asubuhi.
Mreno huyo aliwasili mjini Turin jana Jumapili akiwa na ndege yake binafsi na leo Jumatatu asubuhi alifika J Medical Centre karibu na Uwanja wa Allianz kwa ajili ya vipimo hivyo.
Ronaldo alisaini jezi kwa mashabiki waliokuwa wakimsubiri na huku wakiimba jina lake. Endapo atafuzu kwa vipimo Ronaldo (33) atambulishwa rasmi kuwa mchezaji Juventus jioni ya leo.
Katika muda wa mchana Ronaldo atakutana na kocha Juventus, Massimiliano Allegri na wachezaji wenzake wapya kukamilisha uhamisho wake kutoka Real Madrid.
Mashabiki wa Juventus walijitokeza nje ya hospitali tangu asubuhi kwa ajili ya kumuona shujaa wao mpya wakiwa na bango yao pamoja na jezi ‘Ronaldo 7’.
Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...
By Mwandishi WetuApril 16, 2024Spread the love IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...
By Mwandishi WetuApril 15, 2024Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...
By Mwandishi WetuApril 15, 2024Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...
By Masalu ErastoApril 15, 2024
Leave a comment