Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Corona isiwe kigezo watoto kukosa chanjo
Habari Mchanganyiko

Corona isiwe kigezo watoto kukosa chanjo

Dk. Ahmad Makuwani, Mkurugenzi Msaidizi Afya ya Uzazi na Watoto
Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imeitaka jamii kutotumia kipindi hiki cha maambukizi ya virusi vya corona (Covid-19) kama kigezo cha kutopeleka watoto kwenye chanjo ili wapate kinga ya magonjwa mengine. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Rai hiyo imetolewa jana Jumatatu tarehe 22 Juni 2020 na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Watoto, Dk. Ahmad Makuwani kwenye semina ya waandishi wa habari wa Mikoa ya Singida na Dodoma kuhusu huduma za chanjo nchini.

Alisema maambukizi ya corona kwasasa yamepungua na kuwataka Watanzania kutotumia ugonjwa huo kama sababu ya kutowapeleka watoto kupata chanjo.

“Tulikuwa tunaenda vizuri lakini hivi karibuni idadi ya watoto na wasichana wanaopaswa kupata chanjo ya mlango wa kizazi imepungua, hizi chanjo ni muhimu sana, jamii ipeleke watoto kwenye vituo wapate chanjo” alisema Dk. Makuwani.

Alibainisha, Tanzania imepiga hatua kwasasa katika utoaji wa huduma za chanjo huku akidai kuna vituo zaidi ya 600 vinavyofanya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi.

“Tunaamini mtatumia weledi wenu kuelimisha jamii kuhusu huduma ya chanjo mbalimbali zinazotolewa, wahimizeni wananchi kule vijijini wapeleke watoto wao kwa kuwa chanjo inatolewa kwenye vituo vya kutolea huduma” alisema Dk. Makuwani.

Alisisitiza waandishi waendelea kuhamasisha wananchi kunawa mikono kwa kuwa imesaidia kupunguza kasi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Awali, akizungumzia hali ya huduma za chanjo nchini, Ofisa Programu ya Chanjo wa Mpango wa Taifa wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya, Lotalis Gadau, alisema pamoja na jitihada za kuhakikisha magonjwa yanayizuilika kwa chanjo yanapewa kipaumbele kwa kuwapatia watoto chanjo lakini bado kuna jamii hazichanji watoto.

“Baadhi ya chanjo kiwango kipo chini ya kiwango kinachotakiwa, chanjo ya Surau na Rubella kitaifa tuna asilimia 76% ambayo iko chini ya kiwango cha utoaji wa huduma za chanjo ambayo inatakiwa kuwa asilimia 90,” alisema Gadau kupitia tathmini ambazo hufanywa na wizara kuona hali ya huduma za chanjo.

Alisema kuwepo kwa ugonjwa wa corona sio sababu ya kutopeleka watoto kupata chanjo kwasababu wakichanjwa inasaidia kuwakinga na magonjwa mengi zaidi.

Alisema wizara imekuwa ikifanya usimamizi elekezi wa huduma za chanjo katika kipindi ambacho mlipuko wa ugonjwa wa corona ulivyoanza na shule kufungwa kuona hali ya utoaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi (HPV).

Alisema kwenye jamii ambapo wananchi wengi wamekuwa wakiogopa kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya wakiogopa maambukizi na kuihamasisha jamii kwenda kupeleka watoto wao kupata chanjo hizo muhimu huku wakizingatia tahadhari za kujikinga na ugonjwa wa corona.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!