Kamishna Msaidizi wa Polisi, Wankyo Nyigesa (katikati)

Coaster lagonga lori sita wafariki papo hapo

WATU sita wamepoteza maisha huku saba wakijeruhiwa katika ajali ya basi la abiria iliyotokea leo tarehe 6 Novemba 2018 maeneo ya Segera mkoani Tanga. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza kuhusu ajali hiyo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Wankyo Nyigesa amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari la abiria aina ya Coaster lenye namba za usajili T124 DHW kugonga kwa nyuma lori lililoegeshwa kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo.

Kamanda Wankyo amesema lori hilo lenye usajili wa namba za nchi jirani, liliegeshwa kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo katika barabara ya Segera.

Aidha, Kamanda Wankyo amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Bagamoyo.

WATU sita wamepoteza maisha huku saba wakijeruhiwa katika ajali ya basi la abiria iliyotokea leo tarehe 6 Novemba 2018 maeneo ya Segera mkoani Tanga. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Akizungumza kuhusu ajali hiyo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Wankyo Nyigesa amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari la abiria aina ya Coaster lenye namba za usajili T124 DHW kugonga kwa nyuma lori lililoegeshwa kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo. Kamanda Wankyo amesema lori hilo lenye usajili wa namba za nchi jirani, liliegeshwa kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo katika barabara ya Segera. Aidha, Kamanda Wankyo amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram