Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chuo cha Diplomasia kimenufaisha 3,421
Habari za Siasa

Chuo cha Diplomasia kimenufaisha 3,421

Spread the love

JUMLA ya wanachuo 3,421 wamehitimu masomo yao katika Chuo cha Diplomasia tangu kuanzishwa kwake mwaka 1978. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 23 Aprili 2019 na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrka Mashariki, Damas Ndumbaro wakati akijibu swali la Mbunge wa Malindi, Ally Salehe Ally (CUF).

Katika swali lake Salehe alitaka kujua Chuo Cha Diplomasia kimetoa wahitimu wangapi tangu kuanzishwa kwake mwaka 1978?

Ndumbaro amesema, wahitimu wa ngazi ya Shahada ni 72, Stashahada  ya Uzamili katika Menejimmenti ya Mahusiano ya kimataifa  ni 503, Shahada uzamili katika Diplomasia ya Uchumi ni 341, Stashahada ya kawaida 2084, ngazi ya cheti ni 347 ni wa mafunzo maalum ya maafisa waandamizi wa Mambo ya Nje.

Amesema, katika idadi hiyo ya wahitimu katika Chuo cha Diplomasia wanawake 1,060 na wanaume 2,361.

Naibu huyo amesema, wanafunzi hao walitoka nchi mbalimbali ikiwemo Afrika Kusini, Algeria, Angola, Butswana, Burundi, Jamhuri ya Kongo, Guinea, Kenya. Comoro, Libya, Malawi na Msumbiji.

Nchi zingine ni pamoja na Namibia, Palestina, Rwanda, Sudan, Zambia, Zimbabwe pamoja na hapa nchini.

Amesema kuwa, tangu kuanzishwa kwa chuo hicho mpaka sasa, wanachuo 500 kutoka Tanzania wamehitimu na kufanya kazi katika maneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Na kwamba, kutokana na umuhimu wa lugha za kufundishia, chuo kwa sasa inafundisha kwa kutumia ya lugha mbalimbali za kigeni katika kufundishia.

Ametaja lugha hizo kuwa ni pamoja na Kifaransa, Kihispania, Kingerreza, Kikorea na Kireno.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!