June 22, 2021

Uhuru hauna Mipaka

China yaidhinisha nyongo ya dubu kutibu corona

Dubu

Spread the love

TAIFA la China limeidhinisha matumizi ya nyongo ya dubu kuwatibu wagonjwa wa  corona (COVID-19). Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Kwa kujibu wa taarifa ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC Swahili), China imeeleza nyongo ya dubu – ambayo ni kimiminika kinachosaidia kusaga chakula huchukuliwa kutoka kwa dubu ambao ni hai – imekua ikitumika kwa muda mrefu nchini humo kama dawa ya kienyeji.

Nyongo hiyo ambayo ina tindikali ya ursodeoxycholic, hutumiwa kuyeyusha mawe yanayojitengeneza katika kibofu cha mkojo na kutibu ugonjwa wa maini.

Taarifa ya bbc imeeleza, hakuna uthibitisho kuwa ina ufanisi dhidi coronavirus na mchakato wa kuitoa huwasababishia machungu sana wanyama hao.

Brian Daly, msemaji wa wakfu wa Animals Asia Foundation, aliliambia shirika la habari la AFP kuwa “hatupaswi kuwa tunategemea bidhaa za wanyama kama nyongo ya dubu kama suluhu ya kukabiliana na virusi vinavyoua ambavyo vinaonekana kuwa asili yake ni wanyamapori.”

Pia baadhi ya miji ya China imeanza kubadili mwelekeo kwa kupiga marufuku ulaji wa mbwa na paka.

Mji wa Shenzhen, umekuwa mji wa kwanza nchini humo kupiga marufuku ulaji wa nyama za mbwa na paka. Ni kwa kuwa, msingi wa mlipuko wa corona nchini humo umehusishwa na ulaji wa wanyamapori. Sheria hiyo itaanza kutekelezwa tarehe 1 Mei 2020.

Taarifa kutoka shirika la kutetea haki za wanyama, Humane Society International (HSI) limeeleza, mbwa 30,000,000 hufanywa kitoweo katika bara la Asia.

“Mbwa na paka kama wanyama wa nyumbani wameweza kuwa na uhusiano wa karibuu sana na binadamu kuliko wanyama wengine wote. Kupiga marufuku ulaji wa nyama za mbwa na paka na wanyama wengine wa nyumbani ni jambo la kawida katika mataifa yaliyoendelea na kama miji ya Hong Kong na Taiwan,” ilisema serikali ya jiji la Shenzhen kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la Reuters.

“…kusema ukweli ni mafanikio makubwa katika juhudi za kumaliza ukatili huu ambao unakadiriwa kuwauwa mbwa milioni 10 na paka milioni 4 nchini China peke yake kila mwaka,” alisema Dk. Peter Li, mtaalamu wa sera katika kampuni ya China ya HSI.

error: Content is protected !!