Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CHAUMMA yataka uwazi taarifa za corona, waathirika wafidiwe
Habari za Siasa

CHAUMMA yataka uwazi taarifa za corona, waathirika wafidiwe

Hashim Rungwe, Mwenyekiti wa Chama cha Umma
Spread the love

CHAMA cha siasa cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) nchini Tanzania, kimeitaka Serikali nchini humo kutoa takwimu mara kwa mara, kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Zaidi ya siku 10 zilizopita, Serikali ya Tanzania haijatoa takwimu za mwenendo wa Covid-19. Mara  ya mwisho takwimu hizo zilitolewa tarehe 29 Aprili 2020 na Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wan chi hiyo.

Hata hivyo, tarehe 8 Mei 2020, Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya wa Tanzania, alisema Serikali imesimama kutoa takwimu hizo kutokana na maabara inayopima Covid-19, kufanyiwa marekebisho, ambayo yatakamilika ndani ya muda mfupi.

Waziri ummy alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku tano tangu alipomwelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Profesa Mabula Mchembe kuwasimamisha kazi mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, Dk. Nyambura Moreni na Jacob Lusekelo, Meneja Udhibiti wa Ubora ili kupisha uchunguzi.

Uamuzi huo wa Waziri Ummy ulikwenda sambamba na kuunda kamati ya wataalamu wa afya yenye watu kumi inayoongozwa na Profesa Eligius Lyamuya wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Kamati hiyo inapaswa kukabidhi ripoti kwa Waziri Ummy, tarehe 13 Mei 2020.

Akizungumza leo Jumatatu tarehe 11 Mei 2020, na MwanaHALISI Online kwa simu,  Eugine Kabendera, Naibu Katibu Mkuu Chaumma Bara amesema, taarifa za mwenendo wa ugonjwa huo zikitolewa, wananchi wataongezeka umakini katika kuchukua tahadhari zinazotolewa na watalaamu wa afya, juu ya kujikinga na mamabukizi yake.

“Ni haki yetu tupate taarifa ya hali ya afya inavyoendelea, ili kila mmoja unaposema watu wajitenge wavae barakoa watafanya, ukikaa kimya watu hawawezi kuona umuhimu wa kuchukua tahadhari,” amesema Kabendera akijibu swali aliloulizwa anaonaje mwenendo wa COVID-019 unavyoendelea nchini

Wakati huo huo, Kabendera imeishauri Serikali iingilie kati suala la baadhi ya wafanyakazi wa sekta binafsi, wanaoshindwa kulipa mshahara wafanyakazi wao kutokana na athari za janga la Corona.

Kabendera ameishauri Serikali kuhakikisha mifuko ya hifadhi ya jamii, inatoa fedha za kufidia wafanyakazi wasiolipwa mshahara wakati huu.

“Rais amezungumza na amewahakikishia waalimu watalipwa mishahara yao na wanaendelea kulipwa, lakini taasisi binafsi wafanyabiashara wanajiendesha kwa kutumia ada. Mzazi hawezi kulipa ada hali inayopelekea baadhi ya walimu wanalipwa nusu,” amesema Kabendera

“Serikali ina wajibu kuingilia kati na si kwa kushinikiza waajiri kulipa, lakini wafanyakazi wanakatwa pesa kwenda katika mifuko ya kijamii ili kufidia majanga kama haya. Serikali iingilie kati ili iweze kufidia janga hilo.”

Tarehe 17 na 18 Machi mwaka huu, Serikali ya Tanzania ilifunga shule kwa muda wa mwezi mmoja, vyuo vya kati na vikuu pamoja na taasisi ya elimu, ili kudhibiti ueneaji wa Covid-19.

Baada ya muda huo kupita, Waziri Majaliwa alisema agizo la shule na vyuo kufungwa, litaendelea hadi pale Serikali itakapotoa taarifa nyingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!