Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yatoa kauli kushambuliwa Mbowe
Habari za Siasa

Chadema yatoa kauli kushambuliwa Mbowe

John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimelitaka Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama nchini Tanzania, kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio la Freeman Mbowe, mwenyekiti wake, kushambuliwa na watu wasiojulikana. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe, ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ameshambuliwa usiku wa kuamkia leo Jumanne tarehe 9 Juni 2020, wakati akirejea nyumbani kwake Area D jijini Dodoma.

Kwa sasa Mbowe anatibiwa katika Hospitali ya DCMCT Ntyuka jijini humo, ambapo baadae anatarajiwa kuhamishiwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Akizungumzia tukio hilo makao makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Jumanne tarehe 9 Juni 2020, John Mnyika, Katibu Mkuu wa chama hicho amesema, vyombo vya ulinzi na usalama vinapaswa kufanya uchunguzi wa haraka juu ya tukio hilo, ili hatua stahiki zichukuliwe kwa waliohusika.

“Natoa wito kwa jeshi la polisi na vyombo vya ulinzi na usalama vilichunguze jambo hili kwa mapana na mawanda yake yote,  ili waliohusika wafahamike kwa haraka ili hatua za haraka zichukuliwe,” amesema Mnyika.

Aidha, Mnyika amelitaka Jeshi la Polisi kufanyia uchunguzi kauli zilizotolewa na baadhi ya watu kuhusu viongozi wa upinzani kushambuliwa, siku kadhaa kabla ya tukio hilo kutokea.

“Milango hii ya uchaguzi waifungue kwa upana wake sababu siku chache kabla kushambuliwa kulisambaa video kwenye mitandao ya kijamii ikimnukuu mtu aliyejiita mchungaji wa kitaifa Mashimo akizungumza maneno yenye kuashiria kuna tukio litatokea mbele la  kiongozi wa upinzani kushambuliwa ,” amesema Mnyika

“Kati ya majina aliyotaja ni mwenyekiti Mbowe, hivyo kama wanataka kufanya uchunguzi wa ukweli watambue kuna kauli zilitolewa kabla, polisi wamkamate mchungaji aeleze hizo taarifa alizipata wapi.”

Aidha, Mnyika amesema, Chadema inaendelea kufuatili kwa ukaribu tukio hilo na kwamba watatoa taarifa zaidi baada ya ufuatiliaji hao kukamilika.

“Sisi kama chama tunaendelea kufuatilia kwa karibu, kipaumbele chetu kwa sasa ni kuhakikisha anapata matibabu yanayostahili ngazi zote, baada ya ufuatiliaji wetu wa tukio hili, tutakuja kuwaeleza masuala ya ziada na hatua nyingine ambazo chama zitasema ili zichukuliwe, “ amesema Mnyika.

Akijibu swali aliloulizwa kuwa Mbowe wakati anashambuliwa alikuwa na nani, Mnyika amesema, “hakuwa peke yake katika eneo ambalo tukio lilitokea, tunaendelea kufuatulia na kwa wakati mwafaka tutazungumza.”

Pia, Mnyika amepinga kitendo cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto aliyesema tukio hilo lisihusishwe kisiasa akisema, waliomshambulia Mbowe walitoa kauli zinazoashiria mambo ya kisiasa.

Amesema, watu hao waliomshambulia Mbowe, walikuwa wakisema, “hatudhamilii kukuua, lakini pamoja na kutamka maneno hayo, walikuwa na silaha ambazo hawakuzitumia. Walimshambulia maeneo mbalimbali ya mwili na eneo lililoathirika zaidi ni mguu wake wa kulia.”

Endelea kufuatilia MwanaHALISI ONLINE kwa habari zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!