Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yasubiri Corona ipite, kuliamsha upya
Habari za Siasa

Chadema yasubiri Corona ipite, kuliamsha upya

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

MIKUTANO ya ndani na hadhara iliyopangwa na Chama cha Demokrasia na Maebdeleo (Chadema), kuanza tarehe 4 Aprili 2020, sasa haitafanyika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hatua hiyo imeelezwa ni kutokana na kuwepo kwa tishio kubwa la kusambaa kwa virusi vya homa ya mapafu (COVIC-19), vinavyoitesa dunia kwa sasa.

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 23 Machi 2020, Freeman Mbowe, Mwenyekiti chama hicho Taifa na Mbunge wa Hai, amewataka viongozi wa ngazi zote wa chama hicho, kusubiri mpaka janga hilo litakapokoma.

“Wataalamu wetu wametoa utaratibu mwingi, miongoni mwa maelekezo makuu ni kukwepa mikusanyiko mikubwa, tutaahirisha shughuli zote za mikusanyiko mikubwa, tutashirikiana na Watanzania wenzetu kuhakikisha tunapambana kikamilifu na janga hili, nawaomba viongozi watoe ushirikiano na jamii inayowazunguka,” ameagiza Mbowe na kuongeza:

“Siku chache zilizopita baada ya kutoka gerezani, nilipozungumza Dar es Salaam kabla serikali kutangaza kuwepo kwa mgonwja wa corona, nilitangaza na kutoa maelekzo kwa viongozi wa chama ngazi mbalimbali, wajiandae kuanza mikutano ya hadhara kuanzia tarehe 4 Aprili 2020, ili kupaza sauti ya ulazima wa Tume Huru ya Uchaguzi, pili kukiandaa chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu,

“Kauli ile niliitoa wakati serikali haijatangaza uwepo wa mgonjwa wa corona, lakini tangu kipindi kile wagonwja wameshazidi 12, kwa kuangalia historia ya mataifa mengine.

“Mlipuko wa corona ni hatari sana, kwa waliopuuza wamejikuta katika gharika kubwa sababu ukizidi watu 10 unakuwa na hatari sana kiafya.”

Wakati huo huo, Mbowe ameishauri serikali kufunga mipaka ili kudhibiti ueneaji wa ugonjwa huo.

“Kama kweli ni sahihi kuacha wazi mipaka ili kuingiza utalii kwa ajili ya kupata mapato kupitia utalii , Rwanda inafunga mipaka, sisi tunamsubiri nani aje atuambie tuifunge mipaka?

“Tutakuja kufunga mipaka wakati watu wetu wanakufa kama kuku. Ndio tufunge mipaka, itakua tumechelewa sana,” amesema Mbowe.

Mbowe ameishauri serikali kuhakikisha vipimo vya ugonjwa huo vinapatikana katika hospitali za mikoa yote.

“Serikali isione aibu kukabiliana na jambo hili, sisi tuko tayari kushirikiana na serikali, hili jambo ni la watu wote, hatua za makusudi zichukuliwe, vipimo vya corona vifanyike katika hospitali zote tena vya haraka, sababu tunayochelewa kutoa majibu maambukizo yanaongezeka kwa kasi,” ameshauri Mbowe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!