Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yapewa somo la wagombea uchaguzi mkuu 
Habari za Siasa

Chadema yapewa somo la wagombea uchaguzi mkuu 

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Mwendeleo (Chadema) nchini Tanzania, kimepewa mbinu za ushindi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Wabunge, Madiwani na Rais Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbinu hizo zimetolewa leo Jumamosi tarehe 13 Juni 2020 jijini Dar es Salaam, na Dk. Azaveli Lwaitama, Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Dk. Lwaitama alikuwa akizungumza katika mkutano ulioitishwa na Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo kupitoa Chadema aliowakutanisha wadau wa jimbo hilo kuwaeleza mafanikio ya miaka mitano ya ubunge wake.

Mwanazuoni huyo amekishauri  chama hicho kuchagua wagombea wanaokubalika na wapiga  kura, badala ya kuchagua wagombea wanaopendwa na viongozi wa Chadema.

Dk. Lwaitama amesema, wapiga kura wengi hawana chama, hivyo wakati wanapiga kura huangalia mtu wanayemtaka na si chama cha siasa.

“Wako wengi kwenye suala hili ambao pia wengine sio wanachama wa Chadema. Kama unataka kushinda kupitia wanachama wa Chadema bado hujaelewa. Wananchi wengi hawana vyama, sababu watu wanachagua mtu hawachagui chama,” amesema Dk. Lwaitama.

Dk. Azaveli Lwaitama, Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) 

“Ukijua hilo mgombea wako atashinda na atachaguliwa na watu wa vyama mbalimbali. Mtu atachaguliwa kwa sifa zake ikiwemo kuwa karibu na wapiga kura wake,” amesema

Akisisitiza hoja yake, Dk. Lwaitama amekumbushia matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, ambapo amesema Edward Lowassa, aliyekuwa mgombea wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), alipigiwa kura na wanachama wa CCM.

“Kuteua mgombea wa hovyo hata chaguliwa hata kama watu wanakipenda chama chako. Hata Lowassa alipigiwa kura na WanaCCM na hata wao wanajua,” amesema Dk. Lwaitama.

“Msimamishe yule ambaye wa Ubungo wanamtaka, ukimsimamisha yule Chadema anayemtaka hujaelewa. Wasikilize watu wa Ubungo wanataka nini,” Dk. Lwaitama.

Wakati huo huo, Dk. Lwaitama amewashauri wananchi kipindi cha upigaji kura, wachague mgombea bora bila kujali anatoka chama gani.

“Kwa wanachama wa vyama vingine, ujumbe wangu ni huu unapokwenda kupiga kura usifumbwe na chama angalia na mpime aliyetia nia akateuliwa na chama fulani,” amesema

Mpigie chapuo kwa sababu unaona matatizo ya jimbo lako anayabeba na hana ubaguzi sababu kama ana ubaguzi hatakusaidia sababu wananchi wa ubungo hawana chama kimoja,” amesema Dk.  Lwaitama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

error: Content is protected !!