Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yamuunga mkono Maalim Seif, kuachiana majimbo na kata
Habari za Siasa

Chadema yamuunga mkono Maalim Seif, kuachiana majimbo na kata

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kumuunga mkono Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, pamoja na kuachiana majimbo na kata na chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Uamuzi huo umetangazwa leo Jumapili tarehe 4 Oktoba 2020 na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema wakati anatangaza maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho, iliyoketi jana Jumamosi jijini Dar es Salaam.

Maalim Seif Sharrif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

Mbowe amesema, uamuzi huo umekuja baada ya  Mgombea Urais wa Chadema Zanzibar, Said Issa Mohammed kuridhia kujitoa katika kinyang’anyiro hicho na kumuunga mkono Maalim Seif.

 

“Sisi kama Kamati Kuu jana tumeamua na kuridhika na kauli za viongozi wa vyama vyetu hususan Chadema na ACT baada ya kushauriana kwa kina na mgombea wetu wa Zanzibar tumeona ni sahihi chama chetu kumuunga mkono Maalim Seif na kwa maana hiyo anaridhia kujitoa kwa hiari yake,” amesema Mbowe

Mbowe amesema, Kamati Kuu za Chadema na ACT-Wazalendo ziko katika utaratibu wa kutafuta namna watakavyoshirikiana katika Uchaguzi wa wabunge na madiwani kwa pande zote mbili, Tanzania Bara na Zanzibar.

“Chama chetu kimeona umuhimu wa ushirikishwaji wa ngazi mbalimbali za chama katika kuungana kwenye kusimamisha wagombea wa ubunge na udiwani, tumeziachia kamati (za Chadema na ACT-Wazalendo) kufanya mazungumzo kwa haraka kuona tunaachianaje majimbo na kata,” amesema  Mbowe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!