Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yakumbwa na msiba mzito
Habari za SiasaTangulizi

Chadema yakumbwa na msiba mzito

Spread the love

MWALIMU Kasuku Bilago, mbunge wa Buyungu, wilayani Kakonko, mkoani Kigoma (Chadema), amefariki dunia. Anaripoti Saed Kubenea kutoka Dodoma…(endelea). 

Mwalimu Bilago amekutwa na mauti mchana wa leo Jumamosi,  wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Taaarifa za kifo cha mwanasiasa huyo wa upinzani nchini, zimethibitishwa na mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na ofisi ya katibu wa Bunge mjini hapa.

Mwalimu Bilago alifikishwa Muhimbili Jumatano iliyopita – tarehe 23 Mei – kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa kujikunja kwa utumbo.

Akizungumzia msiba huo, mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Zuberi Kabwe amesema, amepokea kwa mshutuko mkubwa kifo cha Mwalimu Bilago.

Amesema, “…Kigoma tumepata pigo lingine. Mwalimu Kasuku Bilago, amefariki dunia. Ni uchungu usioelezeka kumpoteza kiongozi huyu aliyekuwa na mapenzi ya dhati kwa mkoa wetu, nchi yetu na taaluma ya ualimu.”

Anasema, “Mungu amlaze mahala pema peponi ndugu yetu…”

Mwalimu Bilago alisafirishwa na uongozi wa Bunge kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi, kufuatia hali ya yake kuzidi kudhoofika mara kwa mara.

Mwalimu Bilago amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo uliochukua maisha yake kwa takribani wiki tatu zilizopita.

Kabla ya kusafirishwa jijini Dar es Salaam, alilazwa katika hospitali yamadhehebu ya dini ya Kikirsito mjini hapa ambako alifanyiwa upasuaji.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa John Pombe Magufuli (IJPM), mkoani Dodoma, Mwalimu Bilago, alisindikizwa na baadhi ya wabunge wenzake pamoja na maofisa kutoka ofisi ya Bunge.

Miongoni mwa wabunge waliokuwapo uwanja wa ndege kumsindiza mbunge huyo katika safari yake hiyo ya mwisho, ni pamoja na mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea; mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na mbunge wa viti Maalum mkoani Dodoma, Immaculate Sware Semesi.

Wengine waliokuwapo, ni mbunge wa Viti Maalum mkoani Geita, Upendo Peneza, mbunge wa Viti Maalum kutoka Zanzibar, Mariam Msabaha na Gimbi Masaba, mbunge wa Viti Maalum kutoka mkoani Simiyu.

Akizungumza kwa taabu wakati akitolewa kwenye gari la wagonjwa ili kupandishwa ndege, Mwalimu Bilago aliwataka wabunge wenzake walioko Dodoma kuendeleza kile alichokiita, “mapambano ya ukombozi wa wananchi.”

Alisema, “…nakwenda Dar es Salaam kupata matibabu. Nawaombeni sana mniombee kwa Mungu ili niweze kupona haraka. Niombeeni ili niweze kuungana nanyi mapema zaidi katika harakati hizi.”

Aliongeza, “ninawaacha hapa nikiwa na ombi moja kwenu. Endelezeni mapamba haya ya kuwakomboa wananchi na udhalimu wa CCM (Chama Cha Mapinduzi) na serikali yake hadi haki ipatikane. Msikubali kurudi nyuma.”

Akijibu kauli ya Bilago, Kubenea alisema, “ondoa shaka. Hatutakuangusha. Tutafanya kama unavyoagiza. Tutakuombea na tutaendeleza mapambano haya.”

Alisema, “nenda katibiwe Mwalimu. Sisi tutafanya pae ulipoishia. Usihofu.”

Tangu kuanza kwa mkutano huu wa Bunge, mbunge huyo wa Buyungu, amekuwa mwiba kwa serikali kutokana na uwezo wake mkuwa wa uchambuzi wa bajeti ya serikali, hasa katika suaa la elimu.

Mathalani, akichangia bajeti ya wizara ya elimu, Bilago ambaye kitaaluma ni mwalimu alieleza kwa kina sababu za wanafunzi wa shule binafsi kufaulu na shule za umma kufanya vizuri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!