Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yaivuruga UVCCM Bahi
Habari za Siasa

Chadema yaivuruga UVCCM Bahi

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Bahi, Hassan Kadoki
Spread the love

BAADA ya Katibu Mstaafu wa Chadema wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma, Melickzedeck Lesaka kutangaza kuuburuza mahakamani uongozi wa UVCCM wilaya ya Bahi kwa kumtangaza kuwa amejiunga na CCM sasa uongozi huo umeanza kuweweseka. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hali hiyo ya kuweweseka kwa uongozi wa UVCCM wilaya ya Bahí umetokana na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya hiyo, Hassan Kadoki kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kujivua lawama hizo na kumwachia kimbembe mchungani wa kanisa la uhamsho, Damiani Mchela aliyetoa taarifa hizo.

Kadoki akizungumza na waandishi wa habari alisema, kuwa hajawahi kumpokea Lesaka kutoka Chadema na kujiunga CCM ila aliwahi kutoa taarifa za Lesaka kwenye mkutano ambao alikuwa mgeni rasmi kutokana na taarifa alizopewa na Mchungaji Mchela ambaye alikuwa kada wa Chadema na kujiunga na CCM.

Kutokana hali hali hiyo Kadoki alimtupia mpira mchungaji Mchela na kumtaka aeleze yeye kilichomsukuma kutoa taarifa kuwa Lesaka naye anaunga mkono juhudu za CCM licha ya yeye kutofika katika mkutano.

Mchungaji Mchela alisema kuwa alitoa taarifa hiyo kutokana na Lesaka kumwambia kuwa anaunga mkono juhudi za CCM na kufurahishwa na viongozi wa Chadema kujiunga CCM hivyo na yeye yupo nyuma na atajiunga muda si mrefu.

Kutokana na hali hiyo mchungaji Mchela alisema, kitendo cha Lesaka kubadilika ni kitendo cha utapeli wa kisiasa na anatakiwa kutoa msimamo kama kweli ameachana na siasa na kuwa mhubiri wa injili au anataka kuchonganisha jamii.

Hata hivyo Mchungani Mchela alisema, haogopi vitisho vyake kuwa ataenda mahakamani huku akieleza wazi kuwa yupo tayari kutoa ushahidi na alivyokuwa akifadhili mikutano ya CCM na kuratibu ili iweze kufanikiwa.

Kwa upande wake, Lesaka ameendelea kusema kuwa dhamira yake ya kwenda mahakamani hipo pale pale na hajawahi kujiunga na CCM.

Mbali na hilo, Kadoki alijinadi kuwa, katika uchaguzi wa serikali za mitaa watahakikisha wanashinda kata zote zilizopo katika wilaya ya Bahi na vitongoji.

Akijinadi kushinda uchaguzi huo alisema, sababu kubwa ya kushinda ni juhudi za Rais John Magufuli kutekeleza Ilani ya CCM ambapo wilaya ya Bahi kwa sasa imepata zahanati pamoja na barabara za kiwango cha lami.

Akiendelea kuzungumza na waandishi wa habari Kadoki alisema, kwa sasa wilaya ya Bahi haina shida na upinzani kwani kwa hatua kubwa wameisha ibomoa ngome ya Chadema baada ya viongozi wa ngazi ya juu kumeguka na kujiunga CCM.

Naye aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Bahi, Mathiasi Lyamumda na kuhamia CCM alisema, yeye alihamia CCM kwa kuandika barua ya kuomba kujiunga na chama hicho baada ya kuona alichokuwa akipigania kinatekelezwa.

“Baada ya uchaguzi nilikaa kwa muda wa miaka mitatu nikitafakari juu ya mwenendo wa siasa na utekelezaji nikagundua kuwa nilichokuwa napigania katika wilaya ya Bahi kimepatikana kwa maana ya ujenzi wa zahanati, umeme na barabara ndipo nilipo amuha kuandika barua ya kuomba kuhamia CCM wala sijanunuliwa,” alisema Lyamunda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!