Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yaibuka mshindi nafasi makamu mwenyekiti
Habari za Siasa

Chadema yaibuka mshindi nafasi makamu mwenyekiti

Spread the love

MWENYEKITI wa Kitongoji cha Namayani wilayani Arumeru, Elias Mollel (Chadema),  ameibuka mshindi wa nafasi ya makamu mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Ngaramtoni, anaandika Mwanadishi wetu.

Uchaguzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki, ulikuwa wa kuwatafuta wenyeviti wapya wa kamati mbalimbali na nafasi ya kiti cha makamu mwenyekiti ambapo uchaguzi wa kuwachagua viongozi hao ufanyika kila baada ya miaka mitatu.

Katika nafasi ya makamu Mwenyekiti mtendaji mkuu wa mamlaka hiyo Sophia Shoko, ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi alimtangaza Elias Mollel (Chadema) kuwa mshindi wa nafasi ya makamu mwenyekiti kwa kupata kura 15 dhidi ya Rose Mollel (CCM), aliyepata kura 10.

Akizungumza na wajumbe wa baraza hilo wakati wa kuomba kura kwa kupewa ridhaa ya kuchaguliwa tena kuongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitatu Mollel alisema ndani ya uongozi wake wa miaka mitatu iliyopita ameweza kufanya mambo mengi ya kimaendeleo kwenye mamlaka hiyo.

Amesema kuwa wakati alipochaguliwa mwanzo hapakuwa na Mamlaka ya Mji Mdogo, lakini kwa juhudi zake, mwenyekiti wa mamlaka na wajumbe wa baraza waliweza kushirikiana kwa pamoja kupiga hatua ya kuwa mamlaka ya mji mdogo.

Hata hivyo, alieleza kuwa baada ya kazi kubwa waliyoifanya madarajio yao ni kutoka kwenye mamlaka ya mji na kuwa halmashauri kamili.

Aidha,  mjumbe mmoja alimuuliza ngombe huyo swali kwa kumuuliza kuwa ni muda mrefu umepita tangu kuchaguliwa kuwa kiongozi na wakazi wa mamlaka hiyo wamekuwa wakikamuliwa kwa kulipa kodi na kukusanya mapato ambayo yanapelekwa Halmashauri ya Arusha DC, lakini wakati wa bajeti wanapangiwa fedha kiduchu je atawashawishi vipi wajumbe kumchagua tena.

Akijibu, Mollel amsema bado mamlaka hiyo ipo chini ya Halmashauri ya Arusha DC na kwa sasa wamekidhi vigezo vya kuwa halmashauri kwani wana idadi kubwa ya kaya, kata na tarafa.
Alisema Wizara ya Tamisemi, inaangalia vigezo hivyo na wamekidhi kwa asilimia 80.

Kwa upande wake mgombea wa CCM aliwaambia wajumbe kilichomsukuma kugombea ni kutokana na makamu mwenyekiti amekuwa hakitumia cheo chake na wadhifa vibaya kwa kuwakandamiza wajumbe wa baraza.

Amesema endapo wangemchagua angesimamia haki, sheria, kanuni na miongozo katika uongozi wake, kwani ndiyo chachu ya kuleta maendeleo ya kweli kwa wananachi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!