Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema watakiwa kuacha ‘ujanja ujanja’ wajenge ofisi
Habari za Siasa

Chadema watakiwa kuacha ‘ujanja ujanja’ wajenge ofisi

Wanachama wa Chadema Kilombero
Spread the love

KATIBU wa Kanda ya Kati wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mbassa ameuagiza uongozi wa jimbo la kilombero kuhakikisha wanajenga ofisi ya chama, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo aliitoa wakati akifanya kikao cha viongozi wa Chadema ni msingi jimbo la Kilombero pamoja na kusikiliza kero za jimbo hilo.

Mbasa amesema kuwa ili chama kiweze kujengeka ni lazima kufanya juhudi za kujitolea sambamba na kujenga ofisi badala ya kutegemea.

Mbassa katika kikao hicho amesema siyo jambo la busara kwa jimbo ambalo linaongozwa na mbunge, mwenyekiti wa halmashauri pamoja na naibu mwenyekiti wote wakitokea Chadema huku wakishindwa kujenga ofisi ya chama na kuendelea kutegemea kodi kutoka kanda au taifa.

Mbali na hilo Mbassa amesema ili kujenga chama ni wajibu wa kila kiongozi na mwanachama kuhakikisha anafanya kazi kwa kanuni na taratibu badala ya kutumia muda mwingi kupika majungu.

Amesema kwa sasa viongozi wengi wa chadema wamekuwa wakishindwa kufanya kazi ya chama na badala yake wanatumia muda wao mwingi kupika majungu ikiwamo kulaumiana jambo ambalo siyo sahihi katika ujengaji wa chama hicho.

Aliwataka wananchama na viongozi wa Chadema kuhakikisha wanasoma katiba ya chama hicho ili kujua misingi na mipaka ya uongozi jambo ambalo amesema litaondoa migogoro ambayo siyo ya lazima.

“Kwa sasa kuna migogoro mingi isiyokuwa ya lazima ambayo inatokana na wanachama pamoja na baadhi ya viongozi kushindwa kusoma katiba ya chama.

“Licha ya kushindwa kusoma katiba na kuielewa bado viongozi wamekuwa wakidharauliana jambo ambalo ni aibu katika uongozi ndani ya Chadema jambo ambalo linasababisha mgawanyiko na mtafaruku,” amesema Mbasa.

Kwa upande wake, mbunge wa jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali katika kikao hicho amekiri kutofanya mikutano ya wananchi na kwamba anajipanga kufanya hivyo.

Lijualikali amesema ameshindwa kuwatembelea wananchi kutokana na misukosuko ambayo amekuewa akikumbana nayo.

“Najua kuwa wapo watu wanaonilaumu, lakini ikumbukwe kuwa mimi ni binadamu wakati mwingine nakosea, lakini viongozi nawaomba sana hasa wa ngazi ya vitongoji na kata kuhakikisha mnaitisha mikutano na kunialika ili niweze kuzungumza na wapigakura masuala mbalimbali ya maendeleo,” amesema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!