Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema wajitosa kumng’oa Prof. Lipumba Buguruni
Habari za Siasa

Chadema wajitosa kumng’oa Prof. Lipumba Buguruni

Saed Kubenea, Makamu Mwenyekiti Kanda ya Pwani (Chadema) akizungumza na Waandishi wa habari
Spread the love

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pwani kimeanzisha operesheni maalumu ya kusaidia Chama cha Wananchi (CUF) kumwondoa Profesa Ibrahim Lipumba katika ofisi za makao makuu ya chama hicho zilizopo Buguruni, Dar es Salaam, anaandika Irene David.

Operesheni hiyo iliyopewa jina la “Ondoa Msaliti Buguruni” (OMB) inaungwa mkono pia na wanachama wa CUF wanaokubaliana na msimamo wa chama chao kuwa Lipumba si mwenyekiti wao.

Lipumba alijivua uenyekiti wa CUF wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015, lakini alirejea na kujivalisha tena uenyekiti huo Septemba mwaka jana, baada ya CUF kuwa imeteua Julius Mtatiro kukaimu nafasi hiyo.

Wakati CUF haitambui uenyekiti wa Lipumba, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kwa shinikizo la serikali, anamtambua Lipumba, na amekuwa akimpa fedha ya ruzuku ya chama hicho kumpatia kinyume cha utaratibu. CUF, ikiongozwa na Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu, imafungua shauri mahakamni dhidi ya Msajili, Lipumba na wafuasi wake.

Kwa mujibu wa Saed Kubenea, makamu mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, uamuzi wa chama hicho kusaidia CUF katika jitihada zake kumngoa Lipumba unalenga kunusuru CUF na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) unaojumuisha Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, na NLD, ambao unashambuliwa na serikali kwa njia mbalimbali.

Kubenea, ambaye pia ni mbunge wa Ubungo, amewaambia waandishi wa habari katika ofisi za kanda hiyo, Dar es Salaam, “sisi kama Chadema kwa umakini kabisa tutawasaidia viongozi wa CUF na wanachama wao kumwondoa msaliti ambaye ni Profesa lipumba, Buguruni.

“Katika hili pia tumeamua kila siku ambayo kesi ya CUF inaendeshwa mahakamani wanachadema tutajitokeza kuisindikiza CUF tunayoitambua,tumekubaliana na mameya wetu wote wa jiji la Dar es Salaam wasitoe ushirikiano kwa mtu yoyote mwenye vimelea vya Lipumba,” amesema.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Dkt. Makongoro Mahanga, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam amesema. Naye alisema, “ Chadema ni washirika wa CUF katika Ukawa. Hivyo tunaamini wanavyoyumbishwa CUF hata sisi hatuwezi kubaki salama.

“Tumeona tunaathirika. Makao makuu ya Chadema yapo katika kanda yetu. Tumejiridhisha kwamba mgogoro huu si kati ya Lipumba na Seif, ni kati ya CUF na dola. Tumeamua kupambana na dola kwa kuanza na hawa wasaliti wakiongozwa na Lipumba.”

Alikuwepo pia Riziki Ngwali, Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni. Alisema, “tunataka pia Watanzania watambue kuwa mgogoro wa dola dhidi ya CUF ni wa kupandikizwa, kwa sababu serikali na vyombo vyake vinatumika.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!