WABUNGE na Madiwani wa Chama cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wameishitaki SErikali ya Tanzania kwa Umoja wa Ulaya juu ya hali ya kisiasa na kushinikiza kupatiwa dhamana viongozi wa chama hicho pamoja na kutahadhalisha usalama wa viongozi hao. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).
Viongozi hao waliongozwa na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbles Lema, Peter Lijualikali, Mbunge wa Kilombero, Joseph Haule mbunge wa Mikumi. Wengine ni Boniface Jacob, Meya wa Ubungo, Patrick Ole Sosopi, Mwenyekiti wa Bavicha na wengine zaidi ya 30.
Viongozi wa chama hicho walikosa dhamana Machi 27, 2018 baada ya viongozi serikali kuzuia dhamana zao.
Lema aliyeongoza msafara huo alisema kuwa wataomba hati tahadhari kwenye ubalozi huo.
Amesema kuwa chama hicho kitawaomba ubalozi huo kusiishie tu kutoa matamko ya kupinga kinachoendelea nchini bali waende mbele zaidi na kwa kuchukua hatua stahiki.
Lema amesema kushikiliwa kwa viongozi wao kunatoa tafsiri kuwa chama chote kimefungwa gerezani licha kuwepo mkakati wa serikali kukifunga chama hicho.
Wakati Wabunge na Madiwani wa Chadema wakiwa Ubalozi wa Umoja wa Ulaya, kesi ya viongozi wao inaendelea Makahama ya Kisutu bila ya watuhumiwa kufikishwa mahakamani hapo.
Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri anasikiliza kesi hiyo na kutoa uamuzi wake juu ya dhamana yao. MwanaHALISI Online itawajuza kinachoendelea.
Leave a comment