Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema waanza kupanga safu yao ya uongozi
Habari za SiasaTangulizi

Chadema waanza kupanga safu yao ya uongozi

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeanza maandalizi ya uchaguzi ndani wa ndani. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Wakati harakati hizo zikiendelea Mwenyekiti wa chama hicho anaendelea kusota mahabusu kutokana kufutiwa dhamana yake kwenye kesi ya kufanya maandamano na kusanyiko kinyume na sheria.

Chama hiko tayari kishawasambaza viongozi wake kwenye mikoa na wilaya mbalimbali nchini.

Maandalizi ya Uchaguzi huo unahusisha viongozi wa matawi, kata, majimbo, mikoa na ngazi ya Kitaifa ulianza mapema Desemba mwaka huu.

John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa chama hicho, amesema kuwa tayari chama hicho kishakamilisha maandalizi ya uchaguzi huo.

Ameeleza kuwa chama kitafanya vikao vya ndani kwa ajili ya kuwapa nafasi wagombea kujinadi.

Amesema kutokana na kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara nchini uchaguzi huo unatumia vikao vya ndani ambavyo hata hivyo katika baadhi ya maeneo vimekuwa kaa la moto huku chama kikiwatumia viongozi wenye ushawishi mkubwa wakiwemo wabunge kuongoza zoezi hilo.

“Huu ni mwaka wa uchaguzi ndani ya chama na ndiyo maana tuko nchi nzima, tumesambaa kwa ajili ya kusimamia ili tuweze kuapata viongozi wazuri kuanzia ngazi ya msingi,” amesema Mrema.

Mbunge wa Kibamba, John Mnyika ameshika majimbo ya Momba, Tunduma, Vwawa, Mbeya Mjini na Vijijini wakati Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa akisimamia majimbo yote ya mkoa wa Rukwa.

Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama ‘Sugu’ anasimamia jimbo la Njombe Mjini.

Desemba 16, 2018 Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA -Zanzibar, Salum Mwalimu alikamatwa na Jeshi la Polisi akiwa mjini Mafinga mkoani Iringa alikokwenda kushiriki moja ya kikao cha ndani akitokea Kanda ya Nyasa, ambapo kiongozi huyo ni moja ya safu iliyopangwa kusimamia chaguzi hizo katika majimbo ya Makambako, Makete, Ismani na Iringa Mjini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!