Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema Singida, wamgeuka Mbowe, wasimamisha mgombea
Habari za SiasaTangulizi

Chadema Singida, wamgeuka Mbowe, wasimamisha mgombea

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoani Singida, kimemgeuka mwenyekiti wao wa taifa, Freeman Mbowe na kuamua kushiriki uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Singida Kaskazini, anaandika Mwandishi Wetu.

Taarifa kutoka Ilongero, jimboni Singida Kaskazini zinamtaja Djumbe David Joseph, kuwa ameteuliwa na chama hicho kugombea ubunge katika jimbo hilo.

Kamati Kuu (CC) ya Chadema, iliyoongozwa na Mbowe, ilitangaza kutoshiriki uchaguzi huo wa tarehe 13 Januari 2018 kwa madai ya “kutokuwapo demokrasia nchini.”

Madai ya Chadema yaliegemea jinsi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ilivyoendesha chaguzi mdogo wa udiwani katika kata 43, tarehe 26 Novemba mwaka huu.

Mbali na Singida Kaskazini, majimbo mengine yanayotarajiwa kufanya uchaguzi mdodgo wakati huo, ni Longido na Songea Mjini.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Singida, mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo, Shaban Limu amesema, chama chake, kimemteua Djumbe David Joseph kupeperusha bendera ya Chadema.

Limu amesema, tayari Jumbe amepitishwa na msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Singida na amepata baraka zote za chama hicho mkoani mwake, kushiriki uchaguzi huo.

Amesema, “hivi ninavyokuambia, tumeshamaliza taratibu zote zinazohitajika. Tumefanya kikao cha kujadili jina la mgombea na tumempitisha ndugu Jumbe kuwa mgombea wetu.”

Anasema, “kinachofuata ni kufanya kikao cha kuweka mikakati ya kampeni. Kesho (Jumatano) na kesho kutwa (Alhamisi), tutaingia kazini kwa kufanya kampeni zitakazokileta chama ushindi katika uchanguzi huu.”

Taarifa zinasema, muda mfupi baada ya kupatikana kwa taarifa kuwa Chadema mkoani Singida kimemsimamisha Djumbe kuwa mgombea katika uchaguzi huo, makao ya chama hicho yaliyoko mtaa wa Ufipa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kilitangaza kutomtambua mgombea huyo.

Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, alitangaza kupitia mitandao ya kijamii kuwa chama chake hakijaweka mgombea katika jimbo hilo.

Mrema alisema, “kwa mjibu wa Katiba ya Chadema, Kamati Kuu ndiyo inayopitisha jina la mgombea wa nafasi ya ubunge na Kamati Kuu haijakutana kufanya kazi hiyo.” Akahoji, “sasa hilo jina limepatikanaje?”

Mrema akaitaka Tume ya uchaguzi kuachana na mchakato wa jina hilo na kuongeza, “chama makao makuu kimeagiza tuletewe taarifa na hatua zitakazochukuliwa kwa watu wote waliohusika na kitendo hicho alichokiita, “cha uhaini” kwa chama chake.

Taarifa ya Chadema imetafsiriwa na wachambuzi wa mambo ya kisiasa kuwa mwanzo mbaya kwa chama hicho katika kutekeleza maajumu yake.

Kumeibuka mvutano wa chini kwa chini kati ya wanachama wanaotaka chama hicho kishiriki uchaguzi huo na wanaopinga uamuzi wa kususia uchaguzi.

Uchaguzi katika jimbo la Singida Kaskazini unafanyika kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Lazaro Nyalandu (CCM).

Nyalandu alitangaza kujivua nafasi hiyo, tarehe 30 Oktoba mwaka huu; akajivua nyadhifa zake zote ndani ya chama hicho tawala, ikiwamo uanachama na baadaye akaamua kujiunga na Chadema.

Mbali na Djumbe, wagombea wengine waliojitosa katika kinyang’anyiro hicho na vyama vyao kwenye mabano, ni Dalphina Patrice Mlewa (CUF), Omari Mohammed Sombi (Alliance for Tanzania Farmers Party), Monko Justein Joseph (CCM), Aloyce Mohammed Nduguta (Ada Tadea) na Mchungaji Samwel Libisu (CCK).

Wagombea hao walitangazwa na msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Singida, Rashid Mandoa, tarehe 18 Desemba 2017 kuwa wamepitishwa kuwania nafasi hiyo baada ya kukidhi vigezo vyote vinavyohitajika.

Mandoa amesema wagombea kutoka vyama vya NRC na UMD wameshindwa kupitishwa kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vya sheria ya a uchaguzi.

Aidha, Mandoa amesema, wagombea kutoka vyama vya United Democrat Party (UDP) na United Democraty Peoples Party (UDPP),  wameshindwa kupitishwa kutokana na kushindwa kurejesha fomu.

Hata hivyo, taarifa zilizopatikana baadaye zinasema, Djumbe ameamua kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kushauriana na viongozi wake katika ngazi ya taifa na mkoa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!