Chadema kwachafuka, watimua madiwani wake – MwanaHALISI Online
Diwani

Chadema kwachafuka, watimua madiwani wake

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wilayani Mbeya, kimetangaza kuwavua uanachama madiwani wake watatu kwa madai ya “utovu wa nidhamu na kukiuka taratibu za chama.” Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Uamuzi huo umetangazwa leo mjini Mbeya na katibu wa chama hicho wilayani humo. Madiwani waliovuliwa uanachama, ni Newton Mwatujobe kutoka kata ya Manga; Godfrey Kagili (Sisimba) na Humphrey Ngalawa (Lwambi).

Hata hivyo, kwa mujibu wa katiba ya Chadema, wilaya, mkoa na hata Kanda, hazina mamlaka ya kufukuza au kuchukulia hatua za kinidhamu madiwani. Mamlaka ya nidhamu ya madiwani, ni Kamati Kuu (CC).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama hicho, mmoja wa madiwani aliyetangazwa kuvuliwa uwanachama ni yule ambaye ameonekana kwenye mitandao ya kijamii akimsifia naibu spika, Dk. Tulia Akcson.

Dk. Tulia anatajwa na baadhi ya watu mkoani Mbeya kuwa amejipanga kumng’oa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu).

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wilayani Mbeya, kimetangaza kuwavua uanachama madiwani wake watatu kwa madai ya “utovu wa nidhamu na kukiuka taratibu za chama.” Anaripoti Faki Sosi ... (endelea). Uamuzi huo umetangazwa leo mjini Mbeya na katibu wa chama hicho wilayani humo. Madiwani waliovuliwa uanachama, ni Newton Mwatujobe kutoka kata ya Manga; Godfrey Kagili (Sisimba) na Humphrey Ngalawa (Lwambi). Hata hivyo, kwa mujibu wa katiba ya Chadema, wilaya, mkoa na hata Kanda, hazina mamlaka ya kufukuza au kuchukulia hatua za kinidhamu madiwani. Mamlaka ya nidhamu ya madiwani, ni Kamati Kuu (CC). Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Faki Sosi

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube