CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania kimeahidi kulipa malimbikizo ya madeni ya watumishi wa umma pamoja na kuwaongezea mishahara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbulu … (endelea).
Ahadi hiyo imetolewa jana Jumatano tarehe 16 Septemba 2020 na Mgombea mwenza wa urais wa Tanzania wa Chadema, Salum Mwalimu wakati akizungumza katika kampeni chauchaguzi huo wilayani Mbulu Mkoa wa Manyara.
Mwalimu alisema, Chadema kikifanikiwa kushinda uchaguzi huo, Serikali yake itapeleka bajeti ya nyongeza bungeni kwa ajili ya kuongeza mishahara ya watumishi wa umma na kuwapandisha madaraja.
Akikazia hoja hiyo, Mwalimu alisema, Serikali ya Chadema italipa fedha za watumishi wote wa umma waliohamishwa vituo vya kazi bila kulipwa stahiki zao.
“Tunafahamu kuna watumishi wa umma waliohamishwa vituo vya kazi bila kupewa stahiki zao, Chadema tunasema tutahakikisha kila mtumishi wa umma aliyehamishwa na hakupewa stahiki zake tunakwenda kulipa,” amesema Mwalimu.
Salimu Mwalimu ni mgombea Mwenza wa Tundu Lissu, ambaye amepewa ridhaa ya Chadema kupeperusha bendera yake katika uchaguzi wa kiti cha Urais wa Tanzania.
Leave a comment