Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema, ACT wapigwa ‘stop’ kuadhimisha siku ya wanawake
Habari za Siasa

Chadema, ACT wapigwa ‘stop’ kuadhimisha siku ya wanawake

zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo
Spread the love

JESHI la Polisi limezuia vyama vya ACT-Wazalendo na Chadema kufanya maazimisho ya siku ya wanawake katika mikoa ya Katavi na Geita. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kwa mujibu wa barua zilizotolewa  katika nyakati tofauti na Jeshi la Polisi wilayani Mpanda mkoa wa Katavi na Jeshi la Polisi mkoani Geita, vyama hivyo vimetakiwa kuungana na serikali katika kuadhimisha siku hiyo, na au kufanya maadhimisho yao siku moja kabla au baada ya tarehe 8 Machi 2019.

Barua iliyotolewa tarehe 6 Machi 2018 na Jeshi la Polisi Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, na kusainiwa na Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo, Maria Kway, imevitaka vyama hivyo kuungana na serikali katika kuadhimisha siku hiyo katika uwanja wa Kashaulili.

“Mkoa wa Katavi tutaadhimisha kwa maandamano yatakayoishia uwanja wa Kashaulli,  kwa kuwa ni siku ya kitaifa ya wanawake haitawezekana kuwepo makundi mawili katika maadhimisho hayo. Nawashauri tuungane pamoja siku hiyo kimkoa au mnaweza kufanya siku moja kabla ya tarehe 8/03/2019 au baada ya tarehe hiyo,” inaeleza sehemu ya barua hiyo.

Wakati huo huo, barua ya Jeshi la Polisi Geita iliyotolewa tarehe 7 Machi 2019 na kusainiwa na Mkuu wa Polisi Wilayani Geita, Ally Kitumbu, vyama hivyo pia vimetakiwa kuungana na serikali katika kuadhimisha siku hiyo katika viwanja vya Bugulula kwa upande wa halmashauri ya wilaya na kwa halmashauri ya mji yatafanyika Soko Jipya.

“Hivyo wanawake wote wanatakiwa wahudhurie maadhimisho hayo katika maeneo hayo. Kwa barua hii ninawazuia kufanya maadhimisho hayo katika ukumbi wa Moyo wa Huruma na badala yake anawake wote waungane na wanawake wenzao katika maeneo hayo yaliyotajwa kiserikali.

Hii ni pamoja na kuzuia kufanya matangazo yoyote yanayohusiana na kufanya maadhimisho hayo kwa itikadi za kisiasa,” inaeleza sehemu ya barua iliyotolewa na Mkuu wa Polisi wilayani Geita.

ACT-Wazalendo ilipanga kufanya maadhimisho hayo mkoani Katavi, wakati Chadema ilipanga kufanya maadhimisho hayo mkoani Geita.

Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe katika ukurasa wake wa Twitter amelaani zuio hilo akiandika kuwa “Jeshi la Polisi sasa limekuwa wapangaji wa namna gani vyama vya Siasa viadhimishe Siku ya Wanawake Duniani. Sisi ACT Wazalendo tumezuiwa Huko Mpanda, CHADEMA wamezuiwa huko Geita. Haya ni Mambo ya hovyo na hayapaswi kutokea kwenye nchi Huru. Kwanini Polisi iwapangie wanawake wa ACT Wazalendo namna ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani?”

“Sisi ACT Wazalendo tulipanga kufanya mjadala Kuhusu haki ya uzazi kwa wanawake kwa sababu vifo vya wanawake wajawazito vimeongezeka sana nchini tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani. Tulitaka kutoa mapendekezo ya suluhisho la hali hiyo ili kupunguza vifo vya wanawake wanapojifungua,” ameandika Zitto.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!