Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CDF Venance: Tupo tayari kukabili uchochezi nchini
Habari za Siasa

CDF Venance: Tupo tayari kukabili uchochezi nchini

Venance Mabeyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania
Spread the love

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo (CDF) amesema, majeshi yamejipanga kukabiliana na vitendo vya uchochezi vinavyohatarisha usalama wa nchi. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Jenerali Mabeyo ametoa kauli hiyo leo tarehe 13 Aprili 2019, wakati akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya Rais, Chamwino jijini Dodoma.

“Tunaendelea kufuatila kauli tata zenye kuashiria ishara za uchochezi ndani ya nchi yetu, tuko tayari kukabiliana na vitendo vyovyote vitakavyotokana na uchochezi huo,” amesema Jenerali Mabeyo.

Aidha Jenerali Mabeyo amezungumzia migogoro inayoendelea katika baadhi ya nchi jirani, akisema kwamba jeshi liko tayari kuliinda nchi endapo migogoro hiyo itaathiri kwa namna yoyote ile Tanzania.

“Migogoro inayofukuta katika nchi jirani inaweza ika (influence ) kuleta hali isiyotabirika katika nchi yetu, nikuhakikishie mheshimiwa (Rais John Magufuli)tuko tayari kuilinda nchi yetu.

“Kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama tuko tayari kulinda wananchi na mali zao, na tuko mstari wa mbele kushirikiana na wenzetu,” amesema Jenerali  Mabeyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

error: Content is protected !!