CCM yapata pigo Mpwapwa

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimepata pigo baada ya kufariki diwani wa chama hicho, Dk. Dustan Dalogo diwani kata ya Ng’ambi wilaya Mpwapwa, Dodoma. Anandika Dany Tibason, Mpwapwa … (endelea).

Akizungumzia kifo hicho katibu wa CCM mkoa wa Dodoma, Albert Mgumba amesema diwani huyo aliumwa na baadaye alipelekwa katika hospitali ya Rufaa mkoani Dodoma ambapo mauti yamemkuta.

Amesema diwani huyo ni kati ya madiwani waliogombania nafasi ya Uenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa japo yeye hakubahatika kupenya.

Aliwataja waliogombania nafasi hiyo, marehemu Dk. Malogo, Mwalimu Honarati Pima na aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti ni  Donard Ng’wenzi.

Mgumba amesema taratibu za mazishi zinafanywa na anatarajiwa kuzikwa kesho saa saba mchana.

Alieleza kuwa taratibu zote zinafanywa na chama kwa kushirikiana na familia na maandalizi yanaenda vizuri na mwili wa marehemu bado upo katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Rufaa mkoani hapa.

Amesema msiba huo umemshtua yeye kama katibu wa chama kwani ni mapema mno na watarazimika kufanya uchaguzi tena.

Naye mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje amesema amesikitishwa na msiba huo kwani ni pigo kwa CCM.

“Sina hata cha kusema inaumiza sana maana ni mapema sana na hapa nipo katika msiba wa diwani wetu ni gharama sana kurudia uchaguzi lakini marehemu pia alikuwa hajakamilisha ndoto zake alizowaahidi wananchi,” amesema Mbunge.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimepata pigo baada ya kufariki diwani wa chama hicho, Dk. Dustan Dalogo diwani kata ya Ng'ambi wilaya Mpwapwa, Dodoma. Anandika Dany Tibason, Mpwapwa ... (endelea). Akizungumzia kifo hicho katibu wa CCM mkoa wa Dodoma, Albert Mgumba amesema diwani huyo aliumwa na baadaye alipelekwa katika hospitali ya Rufaa mkoani Dodoma ambapo mauti yamemkuta. Amesema diwani huyo ni kati ya madiwani waliogombania nafasi ya Uenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa japo yeye hakubahatika kupenya. Aliwataja waliogombania nafasi hiyo, marehemu Dk. Malogo, Mwalimu Honarati Pima na aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti ni  Donard Ng'wenzi. Mgumba amesema taratibu za mazishi zinafanywa na anatarajiwa kuzikwa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Danson Kaijage

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube