Bernard Membe, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Tanzania

CCM yamuonya Bernard Membe

Spread the love

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimemuonya Benard Membe, kutokuwa juu ya katiba ya chama hicho. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Onyo hilo limetolewa leo tarehe 27 Novemba 2019 na Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM,  wakati akizungumza katika mahojiano na kipindi cha Konani kinachorushwa na Kituo cha ITV,  kupitia chaneli yake ya Youtube.

Dk. Bashiru ameeleza kuwa, kama Membe ataendelea kutofuata utaratibu, uongozi wa chama hicho utamlazimisha kufuata utaratibu.

“Membe ni mwanachama mwenye haki ya kikatiba lakini ana wajibu.  Kwa hiyo kama anataka kuwa mwanachama wa CCM kama walivyo wengine, lakini wametupa ushindi tunaojivunia afutae utaratibu. Asipofuata utaratibu, atalazimishwa kufuata utaratibu,” ameeleza Dk. Bashiru.

Hata hivyo, Dk. Bashiru amesema Membe hakuwahi kujadiliwa katika vikao vya chama, licha ya kwamba hakuitikia wito wake, alipomtaka kuonana nae akiwa mkoani Geita.

“Hatukuwahi kumjadili  na kwenye vikao hakuwahi kufika.  Kosa halifi kama jinai, kosa halifi unaweza ukadhani limekufa kumbe ni utaratibu wa wakati. Kupitia kwako, naomba kueleza wana CCM tuko makini kulinda utamaduni wa chama, na wanachama kutii viapo vyao,” amesema Dk. Bashiru.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimemuonya Benard Membe, kutokuwa juu ya katiba ya chama hicho. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea). Onyo hilo limetolewa leo tarehe 27 Novemba 2019 na Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM,  wakati akizungumza katika mahojiano na kipindi cha Konani kinachorushwa na Kituo cha ITV,  kupitia chaneli yake ya Youtube. Dk. Bashiru ameeleza kuwa, kama Membe ataendelea kutofuata utaratibu, uongozi wa chama hicho utamlazimisha kufuata utaratibu. “Membe ni mwanachama mwenye haki ya kikatiba lakini ana wajibu.  Kwa hiyo kama anataka kuwa mwanachama wa CCM kama walivyo wengine, lakini wametupa ushindi tunaojivunia afutae utaratibu. Asipofuata utaratibu, atalazimishwa kufuata…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Regina Mkonde

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!