Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yakaa mguu sawa uchaguzi mkuu 
Habari za Siasa

CCM yakaa mguu sawa uchaguzi mkuu 

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, kimeanza rasmi kujipanga kwa ajili ya kushiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Leo Jumatano tarehe 10 Juni 2020, Kamati Kuu ya chama hicho imekutana Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake, Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Taarifa iliyotolewa na Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM imesema, kikao hicho pamoja na mambo mengine, kimepokea taarifa ambazo ni; Mpango wa Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020. 

“Kamati Kuu kwa kauli moja imeridhishwa na kiwango cha maandalizi ya kuelekeza Uchaguzi Mkuu na kuelekeza kutolewa maramoja kwa ratiba ya mchakato wa ndani wa uteuzi wa wana CCM wanaoomba kupewa dhamana ya uongozi katika vyombo vya Dola,” amesema Polepole.

Pia, kikao hicho, kimepokea Maandalizi ya Mwelekeo wa Sera za CCM kwa Mwaka 2020 – 2030 na Ilani ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

“Kamati Kuu imepokea taarifa ya Maendeleo ya Uandishi wa Mwelekeo wa Sera za CCM kwa Mwaka 2020 – 2030 na kujiridhisha kuwa kazi nzuri imefanyika mpaka ngazi ya Rasimu ya Pili.”

“Kamati Kuu pia imepitia kwa mara ya pili Taarifa ya Uandishi wa Ilani ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na imepongeza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa kujumuisha maoni ya wadau mbalimbali na kuelekeza maandalizi ya mwisho ili Ilani hiyo iwasilishwe katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kwa uamuzi wa mwisho,” amesema

Polepole amesema, kikao kimepokea taarifa ya Serikali juu ya Mapambano ya kuudhibiti ugonjwa wa Corona na hatua ambazo zimechukuliwa kuukabili ugonjwa huo kwa mafanikio makubwa.

“Kikao cha Kamati Kuu (KK) ya Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya Tafakuri ya kina juu ya taarifa ya Serikali, kwa kauli moja kimempongeza John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi imara, msimamo thabiti na usioyumba katika kipindi chote cha mapambano dhidi ya ugonjwa huo,” amesema

“Kamati Kuu na kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inaendelea kutoa rai kwa umma wa Watanzania kuendelea kuzingatia ushauri na maelekezo ya Serikali na wataalam wa Afya, kumtanguliza Mungu kwa maombi na shukrani na kuendelea kuchapa kazi kwa bidii,” amesema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!