Bernard Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

CCM yabariki Membe kufukuzwa, yamsamehe Kinana

Spread the love

HALMASHAURI Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), imeridhia uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kumfukuza uanachama Bernard Membe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Pia, NEC imemsamehe na kumfutia adhabu ya kutoshiriki shughuli za CCM kwa muda wa miezi 18, Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu Mstaafu wa chama hicho.

Membe aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete, alifukuzwa uanachama wa CCM tarehe 28 Februari 2020, huku Kinana akipewa onyo kali, kutokana na makosa yaliyokuwa yanawakabili, ukiukwaji wa maadili na misingi ya CCM.

Wanasiasa hao walipewa adhabu baada ya kusambaa kwa sauti ya mazungumzo yao, wakikosoa kitendo cha viongozi wastaafu kudhauriwa pasina mamlaka husika kuchukua hatua.

          Soma zaidi:-

Kabla ya sauti hizo kuvuja, Kinana na Mzee Yusuph Makamba, walitoa waraka kupinga wastaafu kudharauliwa.

Hata hivyo, katika taarifa ya Kamati Kuu kuhusu kufukuzwa uanachama Membe, ilisema mwanasiasa hiyo alionywa na kupewa adhabu mara kadhaa, lakini alishindwa kujirekebisha.

Aliyekuwa Katibu wa CCM, Abrahaman Kinana

Wajumbe wa  NEC walipitisha azimio hilo baada ya Mwenyekiti wake Rais John Magufuli, kuwasilisha ajenda za adhabu zilizotolewa na Kamati Kuu ya CCM dhidi ya wanasiasa hao, leo Ijumaa tarehe 10 Julai 2020 jijini Dodoma..

Awali, Rais Magufuli aliwashauri wajumbe wa NEC kumsamehe Kinana, kufuatia mwanasiasa huyo kujitokeza hadharani kuomba msamaha.

“Hhivi karibuni mwenzetu mmoja ambaye ni katibu mkuu mstaafu alijitokeza hadharani kule Arusha akaomba radhi, akajutia kwa kitendo alichofanya. Kikubwa zaidi aliomba radhi hadharani, ni kitendo kigumu kwa watu wa kawaida kufanya, inahitaji nguvu ya Mungu kutubu hadharani,” amesema Rais Magufuli.

Halmashauri Kuu ya Taifa NEC

Rais Magufuli amesema, “mimi alinigusa sana na nina hakika ninyi wajumbe mmeguswa sana, alipewa adhabu ya karipio miezi 18, mpaka sasa ametumikia miezi minne mitano nafikiri, sasa niliona wajumbe mumsamehe.”

Kuhusu Membe, Rais Magufuli aliwauliza wajumbe wa NEC kama wanabariki uamuzi wa Kamati Kuu kumfukuza uanachama, ambapo wajumbe hao walikubali.

 “Yule mwingine ambaye sitaki kumtaja jina ameondoka moja kwa moja, ile adhabu mmeikubali ya kumfukuza?” Rais Magufuli aliwaliuliza wajumbe wa NEC, ambao walijibu ndio.

HALMASHAURI Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), imeridhia uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kumfukuza uanachama Bernard Membe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea). Pia, NEC imemsamehe na kumfutia adhabu ya kutoshiriki shughuli za CCM kwa muda wa miezi 18, Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu Mstaafu wa chama hicho. Membe aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete, alifukuzwa uanachama wa CCM tarehe 28 Februari 2020, huku Kinana akipewa onyo kali, kutokana na makosa yaliyokuwa yanawakabili, ukiukwaji wa maadili na misingi ya CCM. Wanasiasa hao walipewa adhabu baada ya…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!